Kaya 2,874 zimehitimu kupokea ruzuku za TASAF wilayani Chemba.
Wilaya ya Chemba imepokea Shilingi bilioni 2.7 kutoka Mfuko wa maendeleo ya Jamii (TASAF) kwa mwaka 2024 na 2025 ambapo kaya 6,990 zenye jumla ya walengwa 23,000 zimenufaika na mpango wa kunusuru kaya masikini.
Hadi sasa (Machi 2025) Kaya 2,874 zimefanikiwa kuinuka kiuchumi na sasa wamehitimu kupokea ruzuku hizo wakati kaya 4,116 zinaendelea kupokea ruzuku ili kuboresha maisha yao na kujikomboa kiuchumi.