Kazi gani ingemfaa zaidi Mh.Magufuli mbali na urais?!

Mpiga ngoma za asili, dereva wa mwendokasi, mwana maigizo kama kina Jangala, mpiga mnada kama vile Yono. Ni nyingi mno lakini hizo ni chache kati ya hizo.
 
Watu wengi wanaichukulia hoja hii kama utani lakini ukiitazama kwa undani ni ya muhimu kitaifa.
Muheshimiwa kama angekuwa Mkurugenzi wa TANROAD kazi hiyo angeifanya kwa ufanisi sana kwani kwa uwezo wake mkubwa wa kukumbuka idadi ya kilometers za Barbara na madaraja anetufaa sana. Na humo hakuna siasa,eneo ambalo haliwezi. Urais wa kidemokrasia ni siasa na usipo iweza siasa ni sawa na Fundi muashi umuajiri kuwa daktari wa binadamu
 
Hata Mods wameileta chit chat,
 
Katika maisha kila mtu aliumbwa kuwa "fulani" ukifanikiwa kuwa uluvyoumbwa uwe, basi kazi yako itakuwa ya wepesi kwako hata kama haitakutajirisha.

Unapofanya kazi isiyo lengo la kuishi kwako, kila kiihusucho huwa ni mchakato kwa hiyo,

Ukimuona Muuguzi ANAKERWA na ukweli au kila aingiapo kazini anakutana na watu wanaolalamika maumivu ama kutojisikia vizuri, ujue aliumbwa kuwa MTU WA MAPOKEZI KWENYE NYUMBA YA KULALA WAGENI.

Unapenda ufanyalo au unafanya uliloumbw?

Kama hukuumbwa kuwa kama unayetaka kufanana naye basi hutokuwa kamwe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…