Kazi ipo ccm

Kazi ipo ccm

Pdidy

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2007
Posts
57,951
Reaction score
32,619


lC.gif
John Bwire​
Novemba 11, 2009
rC.jpg


YANAYORIPOTIWA kusemwa kwenye kikao cha Kamati ya Wazee wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na wabunge wa chama hicho mjini Dodoma yanadhihirisha kitu kimoja: Kwamba kweli kuna ombwe la uongozi nchini.
Na si tu kwamba kuna ombwe la uongozi, lakini pia kumethibitisha jinsi dunia yetu ya siasa ilivyotawaliwa na viongozi wanafiki.
Mambo yanayoelezwa kusemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utawala bora), Sophia Simba kwenye kikao cha Kamati inayoongozwa na Rais Mstaafu, Ali Hassan Mwinyi cha kuchunguza uhasama miongoni mwa wabunge wa CCM na serikali yao, yanadhihirisha yote hayo.
Kwa mujibu wa Sophia Simba, hakuna msafi CCM. Amewarushia madongo hata wabunge wa chama hicho wanaoonekana kuwa msitari wa mbele kupiga vita ufisadi kuwa na wao hawana lolote, ni mafisadi kama hao wanaowatuhumu.
Jumla ya mambo yote hayo ni nini? Ni hali tunayoiona ya taifa kusonga mbele kama gari bovu.
Lakini hii si mara ya kwanza kwa taifa kuogelea katika mawimbi makali. Tulishuhudia hivyo wakati wa Mwalimu Julius Nyerere lakini hali haikuachiwa kuwa mbaya hivi, ilidhibitiwa.
Hatuoni dalili za hali hii kudhibitiwa isipokuwa kuendelea kuwa mbaya zaidi baada ya wabunge wa CCM kuanza kusemana kuhusu hata mambo binafsi yanayotia kinyaa. Hakika kitakachofuata ni kushikana makoo.
Yote hayo yanatokea kwa kuwa ndani ya CCM yenyewe hakuna anayeonekana kuwa na ujasiri, nguvu au nia ya kweli ya kurejesha chama hicho katika mwelekeo sahihi. Na hicho ni chama tawala. kikitikisika, Taifa linatikisika.
Kwamba hakuna anayejaribu kutimiza wajibu wake, mfano mzuri wa jambo hilo ni Waziri Sophia Simba mwenyewe anapoulalamikia utawala bora anaousimamia serikalini kuwa uko ‘likizo.’
Pamoja na mambo mengine, Simba aliripotiwa kusema kwamba baadhi ya viongozi wanaoheshimika walipokea pesa kutoka kwa wanaoshutumiwa kuwa mafisadi ili wagharamie kampeni zao.

Waziri huyo aliripotiwa kumshutumu mbunge wa Simanjiro, Christopher Ole Sendeka kwamba kama sheria zingekuwa zinafuatwa na kuzingatiwa, basi huenda sasa angekuwa matatani kutokana na kukabiliwa na tuhuma zilizomhusisha na kosa la kumpa mimba mwanafunzi. Simba akiwa na dhamana ya utawala bora katika nchi hii, anatuambia nini katika hili? Kwamba Sendeka amefumbiwa macho kwa sababu ni mbunge ila angekuwa mwananchi wa kawaida angeshughulikiwa? Tunasisitiza kwamba ipo haja ya kunusuru Taifa na hali hii ya kuwepo kwa ombwe la uongozi kabla ya mambo hayajawa mabaya zaidi. Tunajiuliza wazee wa nchi hii wako wapi?
hs3.gif
 
Ndg unataka wazee ndiyo wasimame, wewe uko wapi? unataka kusema wewe sauti yako haiwezi kusikika. Ongeza volume ya ujasiri.

uchambuzi wako ni mzuri. Kanyaga twende.
 
Najua kijana unataka tukufikirie japo kaudiwani,tupe cv yako.
 
Back
Top Bottom