Kazi ipo ! Uswis wapo nchini kuwanoa jamaa wa TAKUKURU!

Hivi punde

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2017
Posts
2,554
Reaction score
8,587
Wataalamu na wawezeshaji wa kituo cha kimataifa cha utawala bora cha Basel cha Uswisi wapo nchini kutoa mafunzo kwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru).

Kupitia kituo cha kimataifa cha kusaidia urejeshaji wa mali zilizopatikana kwa njia ya rushwa (ICAR), kituo hicho kinatoa mafunzo ya siku tano kwa Takukuru.
Programu ya mafunzo hayo iliyofunguliwa jana Mei 21, 2018 na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, John Mbungo itahitimishwa Mei 25, 2018.

Mafunzo hayo yanalenga masuala ya uchunguzi na uendeshaji wa kesi za makosa makubwa ya rushwa kwenye mikataba ya ujenzi wa miundombinu na ununuzi wa umma; na mbinu za rushwa na udanganyifu katika mikataba na ununuzi.

Taarifa ya Takukuru inasema mafunzo hayo yanawashirikisha maofisa wa idara zingine ikiwamo Mamlaka ya Kupambana na Rushwa Zanzibar (Zaeca); Mamlaka ya Ununuzi wa Umma (PPRA); Kitengo cha Udhibiti wa Fedha Haramu Tanzania (Fiu); Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP); na Jeshi la Polisi.

Mbungo akifungua mafunzo hayo aliwaeleza washiriki kuwa sehemu kubwa ya bajeti ya nchi huelekezwa kwenye miradi ya maendeleo ambayo utekelezaji wake katika ununuzi umegubikwa na vitendo vya rushwa na unawanufaisha wachache.
 
kuna mama mmoja huko kanda ya ziwa alikua anakopesha na mikataba yenye kumkandamiza mteja lakini pia sidhani kama kwa miaka aliyo anza hiyo biadhara alikua analipa kodi. Now takukuru wamemkalia kooni na ninaomba wasiishie hapo tu waendd mbali kuchunguza watu wengine wa aina hiyo
 
mwizi mwizi tu hata ukimpa nini akiamua kukuibia ataiba tu
 
Siku 5 na gharama zinakuwa kama 1b na mkalimani
Natumaini hamna % hapo
Vijana wapige kazi.
Miaka ya neema hii
 
Wataalamu na wawezeshaji wa kituo cha kimataifa cha utawala bora cha Basel cha Uswisi wapo nchini kutoa mafunzo kwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru).

Kupitia kituo cha kimataifa cha kusaidia urejeshaji wa mali zilizopatikana kwa njia ya rushwa (ICAR), kituo hicho kinatoa mafunzo ya siku tano kwa Takukuru.
Programu ya mafunzo hayo iliyofunguliwa jana Mei 21, 2018 na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, John Mbungo itahitimishwa Mei 25, 2018.

Mafunzo hayo yanalenga masuala ya uchunguzi na uendeshaji wa kesi za makosa makubwa ya rushwa kwenye mikataba ya ujenzi wa miundombinu na ununuzi wa umma; na mbinu za rushwa na udanganyifu katika mikataba na ununuzi.

Taarifa ya Takukuru inasema mafunzo hayo yanawashirikisha maofisa wa idara zingine ikiwamo Mamlaka ya Kupambana na Rushwa Zanzibar (Zaeca); Mamlaka ya Ununuzi wa Umma (PPRA); Kitengo cha Udhibiti wa Fedha Haramu Tanzania (Fiu); Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP); na Jeshi la Polisi.

Mbungo akifungua mafunzo hayo aliwaeleza washiriki kuwa sehemu kubwa ya bajeti ya nchi huelekezwa kwenye miradi ya maendeleo ambayo utekelezaji wake katika ununuzi umegubikwa na vitendo vya rushwa na unawanufaisha wachache.
Ni jambo jema sawa! Jitihada za serikali ya awamu ya 5 inabidi tuziunge mkono! Ili mwisho wa siku tuishi maisha ya kufanana, kama gap litakuwepo basi lisiwe kubwa sana! Tufanane wote tuwe na uwezo wa kusomesha watoto wetu Shule za private.
 
Wangekuja na taarifa ya fedha zilizofichwa huko ingesaidia waache hizo drama zao...
 
Back
Top Bottom