Kazi ngumu sana lakini nasave laki kwa mwezi

Your not serious, miaka mitano kwenye kazi iyo.

Save ikifika 1M tu jilipue na biashara na odds ikiwa kwako mwaka unaofata tu utakuwa unamiliki Biashara mbili, naujue cash ya savingi inaongezeka endelea......
 
Umenishangaza graduate, una save ili upate hela ya kuoa?utabaki kuwa masikini
 
Miaka mitano una save hela ya kuolea?, Dogo mbona unayumba!!!
We zichange ila kwa malengo ya kutafuta biashara ya kukutoa kwenye hizo ajira m
Hayo mambo ya ndoa, hata Bure siku hizi unapata mke
 
Kwaio unadunduliza hela ili ukaoe daah aisee..kweli mtu ni familia aliyozaliwa, shule alizosoma, walimu waliomfundisha, marafiki alioambatana nao...
 
Da kijana kwanza nisijue una umri gani,ila katika maisha hakuna kuchelewa cha mhimu kiu yako katika maisha ,lakni kitenga miaka mitano kwa ajili ya kutafta Hela ya kuoa hiyo haiingii akilini na huyo mke ukimuoa kwa Hela zote mtaanzia wapi maana lazima maisha yaendelee
 
graduate wa kozi gani
 
Binafsi nimependa ukweli na uwazi wako hujaona aibu kuandika yaliyo moyoni mwako, kwa hili itakusaidia kusonga mbele maana tunasonga mbele kwa kujifunza.

Nirudi kwemye mada, nakushauru uendelee kufanya kazi hapo na uendelee kusave as much as possible hata kwa kushindia mihogo. Nina uhakika haitafika hiyo miaka mitano utapata dili ambalo litakutoa hapo wewe kuwa mwaminifu tu kwenye kazi yako na kwenye savings utaona maajabu.

Watu wanaponda hapa unafanya kazi ili upate pesa ya kuolea, amini nakuambia ni watu hawa hawa ukiwaomba mchango wa hali na mali kufanikisha zoezi la kuoa watakukimbia na kukutolea maneno ya hovyo. Heri nguo yako iliyochokaa kuliko nzuri ya kuazima maana haitakusitiri.
Fanya kazi ila kipaombele chako cha kwanza kiwe investments then funga ndoa sasa.
 
Kwaio unadunduliza hela ili ukaoe daah aisee..kweli mtu ni familia aliyozaliwa, shule alizosoma, walimu waliomfundisha, marafiki alioambatana nao...
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Sent from my TA-1024 using Tapatalk
 
Mtoa mada atakuwa mvaa 'makobazi' maana hao jamaa kwa kupenda kuoa ni balaa
 
Nikushauri tu, kazi usiyoipenda usifanye muda wote huo.
Unaweza ukajifanya una chapa kazi utunze hela ukafa kabla hata hiyo miaka mitano haijaisha na maisha yako utakuwa umeishi bila furaha.
Jitahidi utafute kingine cha kufanya tena umesema kabisa kuwa wewe ni graduate una nafasi.
 
Achana na mawazo ya kuweka akiba ili kuoa. Weka akiba ili uongeze mtaji ufanye biashara, utoke kimaisha, ndoa itafuata baadae
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…