Kazi ngumu wape SUMA JKT

Kazi ngumu wape SUMA JKT

kasindaga

Senior Member
Joined
Sep 6, 2013
Posts
165
Reaction score
165
Rais wetu Dkt. Suluhu Hasan tunazidi kukupongeza kwa maono yako, makusudi nadhamira ambayo umeonesha kwa kipindi hiki kifupi cha utawala wako kwa kufanya jambo lililo shindikana tangu nchi ipate uhuru.

Mwangaza wa kutupatia umeme Wilaya ya Kishapu kuipitia REA/Tanesco umeonekana. Suma JKT pamoja na hali mbaya ya kijiografia ikiwemo mvua za mafuriko, barabara kukatika, mabonde kujaa maji na majaruba ya mipunga kujaa maji wanajeshi hawa wanaendelea kujenga Mradi wa umeme vijijini Wilaya Kishapu.

Pasipo na barabara nguzo zinabebwa vifuani pasipopitika magari pikipiki zatumika na mikokoteni. Aidha, tunakushukuru Rais kwa kutuongezea wigo wa mtandao wa umeme wa kilomita moja kwa Kila Kijiji kuongezakilomita mbili zaidi jumla kuwa kilomita tatu.

Mama Samia usikate tamaa umetukomboa tunakuunga mkono hatutakuangusha.Wanajeshi wetu pamoja na matatizo ya kijiografia na tabia nchi tuko pamoja nanyi. Aidha, TANESCO msichoke kutuhudimia maana bila nyie tusingepata huduma hizi.
 
Ungetulia ukaandika vizuri kwa mpangilio inaonekana ulikuwa una hoja ya maana,ila barua yako haina paragraph inaumiza macho kuisoma.

Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app
 
Huu ujinga na upumbavu wa kutojua basic economic principles ndio unaoliangamiza taifa ,unajua ni watu wangapi wamekosa ajira hapo kwa huo uduwanzi wa kutumia hao misukule wa JKT?

Electrical Technicians , engineers na kampuni za wakandarasi wazawa zinakosa kazi kwa akili za kimbumbu kama hizi, ndio akili hizi hizi za kuwanyima tenda wazawa na kuwapa wapuuz wa nje kisa ten percent, force account ya magufuli iliua sekta ya ujenzi na mpaka leo kampuni za wazawa zilizifilisika hazijaweza tena kuinuka.
 
Hata kama ni misukule sisi wananchi wa Kishapu tumekosa nini tangu tupate uhuru hatuna umeme, Barabara, mashule, zahanati?

Aidha REA tenda hii imetangazwa mara ngapi na makandarasi wanaikimbia kutokana na mazingira ya nchi?
Unajua Wilaya hii inachangia kikubwa Pato la Taifa?
 
Mwaka Jana Rais Samia ametoa mabilioni kwa TARURA nchi nzima kuboresha Barabara vijijini na alisisitiza zitengenezwe na wazawa ,sasa kwa takwimu zako baada ya mvua hizi leta matokeo
 
Mwaka Jana Rais Samia ametoa mabilioni kwa TARURA nchi nzima kuboresha Barabara vijijini na alisisitiza zitengenezwe na wazawa ,sasa kwa takwimu zako baada ya mvua hizi leta matokeo
wazawa hawana uwezo wa kujenga barabala ya wakijenga basiazitakuwa na mitala ya kuchepusha maji
 
Rais wetu Dkt. Suluhu Hasan tunazidi kukupongeza kwa maono yako, makusudi nadhamira ambayo umeonesha kwa kipindi hiki kifupi cha utawala wako kwa kufanya jambo lililo shindikana tangu nchi ipate uhuru....
Kushukuru ni jambo jema ila uwasilishaji wa kulialia na mlengwa kutajwa kibinafsi na sio serikali ya CCM inaudhi sana. Serikali ya CCM chini ya mwenyekiti wake Ndugu Rais Hassan, hii hali ya kumtukuza Rais Hassan bila muktadha jumuishi wa kutajwa kwa Serikalii ya CCM sio poa
 
Ungetulia ukaandika vizuri kwa mpangilio inaonekana ulikuwa una hoja ya maana,ila barua yako haina paragraph inaumiza macho kuisoma.

Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app
Kwani kusoma kwako ualimu unataka kila Mtu awe Mwalimu?
Acha umbumbumbu Kuna Watu wanashida ya Umeme wanahitaji umeme hata wakiandika kwa kuchanganya HeRufI ujumbe umefika.
 
Back
Top Bottom