FACEU
Member
- Jan 14, 2022
- 17
- 4
Mheshimiwa Askofu Dr. Josephat Mathias Gwajima ni moja kati ya watu wachache sana kuwahi kutokea Duniani. Mheshimiwa huyu ambaye pia ni mbunge wa Kawe jimbo lilipo jijini Dar es Salaam, amekuwa chanzo cha mabadiliko ya watu wengi kiroho na kimwili kwa kweli MUNGU yupo ndani yake. Naweza kusema kwamba wananchi wa Kawe wamepata bahati sana. Unaweza ukawa unawaza ni bahati gani wameipata, ngoja nikufafanulie.
Mosi, ni moja kati ya wabunge wachache sana mwenye muda mwingi wa kujumuika na kushiriki katika shughuli za maendeleo na wananchi wake. Ni ni mbunge ambaye anatumia muda mwingi sana kuwa na wanajimbo, pia kila wakati utamkuta eneo la jimbo lake akifanya kazi bega kwa bega na wananchi wake.
Pili, ni moja kati ya wabunge mwenye moyo wa kujitoa kifedha na nguvu kwa wananchi wake. Ikumbukwe mbunge analipwa mshahara wake kila mwezi. Ukiona kuwa mbunge anatoa pesa ya mshahara wake kwa ajili ya kufanikisha shughuli ya maendeleo, huyo ni moyo wa kujitoa ambao wanao wachache.
Tatu, ni mjenga hoja mzuri na ana namna yake ya kusimamia hoja vizuri. Ni mbunge ambaye akisimama bungeni hutamani akae haraka, kwa kifupi hachoshi. Hakuna hoja ambayo ataisema itaonekana haina maana kwa taifa hata kwa jimbo lake. Hoja zake zina mashiko sana na manufaa sana. Naweza kusema kuwa wana Kawe huyo ndiye kiongozi sasa.
Nne, ni mwenye msimamo na asiye teteleka kwenye kile anachoambiwa. Ni mbunge asiyeamini katika umaskini. Ukiwa na kiongozi ambaye anahubiri umasikini na kujisifia huyo si kiongozi atakayekufikisha kunakotakiwa. Kuwa na kiongozi mwenye msimamo usioyumbishwa ni vizuri. Kawe isimuachie kiongozi huyu wa thamani.
Hayo ni machache tu kati mengi mazuri ambayo nikiyasema hapa nitakesha.