Kazi tano za kujiajiri kwa mtaji mdogo lakini zikakufanya uwe juu kimaisha

dada26

New Member
Joined
Jul 21, 2021
Posts
1
Reaction score
7
Kwa kipindi hiki ambacho ajira zimekua chache sana wa watu ni wengi sana,unaweza kutoka kwenye wimbi hilo la kukaa bila ajira wala kazi ya kufanya.

KAZI ZIFUATAZO UNAWEZA KUFANYA KWA MTAJI MDOGO LAKINI ZIKAKUINGIZIA KIPATO KIKUBWA.

1.KUFUNGUA MGAHAWA WA CHAKULA
kula ni lazima, bilionea mmoja nchini Tanzania aliulizwa iwapo ingetokea amefilisika na kupoteza kila kitu angefanya biashara gani ili arudi juu, alijibu first priority yake ni kuanza kuuza chakula kwa sababu watu ni lazima wale.
Biashara ya chakula huwa inalipa sana hasa maeneo yenye muingiliano wa watu wengi mfano masokoni, kwenye maeneo ya viwanda, site za ujenzi n.k mahali ambapo watu hawawezi kujipikia.
mtaji wake mdogo.. unaweza ukaanza kupika ukiwa nyumbani kwako ukanunua vyombo vizuri then ukabeba chakula ulichokwisha kupika kwenda eneo husika ukaweka kama ni ile miamvuli mikubwa na viti vichache na ukaanzakuwauzia watu chakula. mtaji huanzia kwenye 500000 na kuendelea kutokana na ukubwa wa biashara yako unavyotaka iwe

2.KUFUNDISHA TUITION
kuna watu wenye ujuzi mbali mbali wemesoma na hawana ajira. unaweza kuanzisha center yako ya kufundisha wanafunzi masomo ya ziada kwa kile ambacho una ujuzi nacho na kujipatia kipato
mtaji hasa ni vitabu na sehemu ya kufundishia, unaweza hata fundishia nyumbani.

3 KUTENGENEZA UNGA WA LISHE BORA
siku hizi wanawake wengi wanajiajiri hivyo wengi huwa busy na wanakosa muda kuandaa unga wa uji lishe kwa watoto.
Kuna aina nyingi sana za unga lishe kutokana na vitu unavyotumika kutengenezea unaweza kuchanganya nafaka zisizozidi nne na ambazo hazijakobolewa (hazijatolewa kiini)na mbegu za maboga wengine wanachanganya na mbogamboga zinakaushwa na kusagwa pamoja na unga.
Ni vyema kujifunza zaidi kuandaa unga lishe kisha utengeneze, ukatafuta vifungashio vizuri na lebo ya kufanyia packaging,ukaanza kusambaza kwa watu na madukani.

4.KUFUNGUA DUKA LA KUUZA NAFAKA
nafaka zikikaushwa vizuri huwa zinakaa muda mrefu bila kuharibika, pia hata hivyo nafaka ni lazima inunulike kwa sababu inahitajika kila siku.
Unaweza kwenda mashambani kujumua kama ni mchele,mahindi, mtama.. then ukatafuta fremu ukauza.. au ukawa unasambaza madukani.

5.KUANZISHA KAMPUNI YA KUZOA TAKA
bado jamii nyingi hasa za mijini zina pata shida sehemu za kupeleka taka taka hasa pale magari ya manispaa yanachelewa au kushindwa kwenda kabisa kukusanya taka majumbani,hii itakulazimu uwe na gari au means yoyote ya kubebea taka kwenye nyumba nyingi kwa wakati mmoja, unaweza pita majumbani, ukawaachia mawasiliano ili taka zikijaa wakutafute then unawatoza pesa kiasi kila unapoenda kuchukua taka na kupeleka kwenye madampo yaliyoidhinishwa na manispaa.

Muhimu kuwa na nidhamu ya Biashara kwenye kila kazi unayotaka kujiajiri, kuwa na matumizi mazuri ya pesa na kuwekeza zaidi kwenye miradi ya maendeleo.
 
Ila apo lazima aangalie location ya biashara asije sema biashara ina faida kwa kuiandika tu
 
Wazo zuri sana
 
Wewe unafanya ipi hapo?

KAZI ni kipimo cha UTU
 
Back
Top Bottom