Nadhani ishu siyo chama. Anayepewa madaraka ndani ya chama, ndiyo tatizo. Kwani hata dini; japokuwa zinahubiri wema, lakini wengine, miongoni mwao wanafanya mambo ambayo hata shetani mwenyewe huwa haamini kama yanaweza kufanywa na wanadamu. Nikupe mifano. Ni kwa nini pope wa Roma alinusurika kupigwa risasi mwaka 1982? Sababu gani zilisababisha hata Kennedy, F (rais wa Marekani) kuuawa?
Majibu ya maswali haya na mengine yanaonyesha ni kwa jinsi gani dini zetu zinatumika kufanya mambo ya siasa na kusahau lengo lake kuu la kuhubiri ufalme wa Mbinguni.
Kwa hiyo, sishangai chama kikiwa kinavurugwa na watu wachache wanaokuwa wanakitumia vibaya na wengine wengi kukubali kufuata na hata kusifia matendo yao hata kama ni mabaya. Haya ni matokeo ya kutokutumia vizuri akili zetu na kuwaacha wengine wazitumie badala yetu. Hivi, tukubadilishana nchi; Watanzania wote wakahamia Marekani na Wamarekani wakaja Tanzania (kila watu waende kama walivyo, bila kuchukua kitu chochote), maisha ya Watanzania hawa wakiwa Marekani, yatakuwa endelevu kimaendeleo (sustainable)?
Think critically.