Kazi ya kuzibua vyoo mshahara 1M/month au kazi ya ofisi nzuri mshahara 500k, utachagua ipi?

Mjina Mrefu

JF-Expert Member
Joined
Dec 6, 2016
Posts
3,045
Reaction score
3,389
Hivi wakuu,

Ndo kwa mfano una shida kubwa ya ajira, na wewe umesoma hadi elimu ya juu.

Umezunguka muda mrefu kusaka ajira ukakosa.

Mara paaap, ukapata mchongo kwenye kampuni ya usafi jijini ktk kitengo cha kuzibua vyoo, alafu unaambiwa mshahara ni million moja kwa mwezi alafu mkataba unapewa wa miaka mitano.

Wakati unawaza kusaini mkataba huo ili uurudishe, unapigiwa simu ktk kampuni fulani kubwa uliyoomba kazi. Unaambiwa umepewa kazi ktk kampuni hiyo, kwenye ofisi nzuri zenye kiyoyozi ila mshahara ni laki tano kwa mwezi. Pia unapewa mkataba wa miaka mitano.

Wewe ungechagua ipi?

Mimi ningechagua kuzibua vyoo tu. Najua wale mabishoo na watoto wa mama wengi wangechagua kwenye kiyoyozi.
 
Wenzio wanaangalia network na wana malengo gani, mjini hapa unaeza kufanya kazi ofisi ya mshahara mdogo ila inakusababishia unapata mishe zinazokuingizia kipato cha ziada.
 
Wenzio wanaangalia network na wana malengo gani, mjini hapa unaeza kufanya kazi ofisi ya mshahara mdogo ila inakusababishia unapata mishe zinazokuingizia kipato cha ziada.
Kazi ya kuzibua vyoo haiwezi kukupatia mpunga wa Ziada?
 
Naona watu hawachagui,wanazunguka majibu yao...
Mm ningechagua kuzibua vyoo, Kwanza hyo kazi haifanyiki kila siku mpk mpigiwe sim kuwa kuna choo kimezibwa,then ningepata muda wa kutosha kufanya mishe mishe zingine kwa mshahara ninaopata.

Philips X2560
 
Yani hapo mzee kinyesi huwezi kukabiliana nacho bila kukitibu. Hapo cha kufanya utakibadili kwanza muonekano kwa madawa mbalimbali na kisha unaweza hata kuingia kusafisha bila wasiwasi.. nazivuba vyoo Binafsi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nazibua vyoo...tena sdhan kama Ni kazi itakayochukua muda mwingi per week.
The rest of the time nafanya mishe nyingine.
Kuna point in life inabidi tu upotezee reputation na uwe selfish.
 
Nachagua kuzibua vyoo.
1: Hata mie kinyesi ninacho na hukishika kila nijisafishapo.
2: Ukizibua Leo utakaa muda mrefu kuziba tena
3: Nitawafundisha usafi Pads zihitadhiwe vizuri kwenye bins.
 
Hakuna kazi ya kuzibua choo yenye huo mshahata
nani kakwambia? we jaribu kununua ile mipira ya kuzibulia harafu zunguka mtaani kama utakosa wateja watatu kwa siku wa shilingi 50,000! kwa kila mteja kwa mwezi unaweza fanya hizo hesabu.
sema hawa watu wanahitaji kupewa mafunzo ya kuthamini kazi yao na kuishi kutokana na kipato.
achilia hiyo je ulishawahi kuuliza wale wanaochoma vimishikaki njiani wanapata kiasi gani kwa siku na kazi wanaanza saangapi halafu linganisha na laki tisa zako ulizoamka saa kumi alfajiri.
 
Ningechagua inayonipa amani maana kuendekeza pesa sana nako. Maisha ni kuridhika na kuwa ma mipangilio hata kwa pesa kidogo. Zibua choo upate mipesa mingi then magonjwa yanakunyemelea

Sent using Jamii Forums mobile app
Kweli kabisaa. Maana mimi nikifanya ya kuzibua hata chakula kitakuwa hakiliki
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…