Wadau, kwanza pongezi kubwa kwa Profesa Gurnah , ushindi wa tuzo ya Nobel kupitia fasihi zake ni wa kupigiwa mfano.
Kikubwa cha kujivunia kupitia maandishi yake ni vionjo vya historia ya ukoloni na athari zake kwa watawaliwa. Bila ya shaka mtunzi aliishi au kupitia madhila hayo katika makuzi na masimulizi ya jamii yake .