Kazi za Maafisa Tarafa ni zipi?

Kazi za Maafisa Tarafa ni zipi?

Popcon

Member
Joined
Aug 12, 2018
Posts
28
Reaction score
12
Mimi leo naomba wanajamvi munifafanulie mamlaka ya Afisa Tarafa Kikatiba au kwa mujibu wa katiba, napenda kujua kwasababu ktk zunguka yangu Mimi kama Mimi nimeshindwa kuwaelewa kabisa.

Sababu ni kwamba baadhi yao wamekuwa hawayajui kabisa mamlaka yao na HIVYO kujikuta wakidili na majukumu hadi ya Wenyeviti wa Vitongoji, watendaji wa vijiji, na hivyo kusababisha mgongano wa kimadaraka.
Pia wamekuwa wakitaka wao wawe wasikilizaji Wa migogoro hata inayowahusu wanandoa, kazi ambazo hawapaswi kuzifanya.

Je, haya ndio majukumu yao?
Kama sio, niziombe mamlaka zao ziwapatie semina elekezi baadhi yao, ili wasijiingize kwenye majukumu yasio yao. Kama kuwakomandi watendaji, Kuwashitaki watendaji kwa Maafisa utumushi na kadhalika.

Naomba kutoa Hoja.
 
Afisa Tarafa ni mkuu wa kamati ya ulinzi na usalama katika tarafa yake na anawajibika kwa mkuu wa wilaya.
 
Hivi eneo ili lipewe hadhi ya Tarafa linatakiwa liwe na sifa gani? Kwa wanaojua please
 
MAJUKUMU YA KAZI
(i) Kwenye Mamlaka ya Serikali Kuu
• Kumwakilisha na kumsaidia Mkuu wa Wilaya katika utekelezaji wa shughuli za Serikali Kuu katika Tarafa.
• Kuandaa na kuratibu taarifa na ripoti zinazohusu masuala ya ulinzi na usalama ya kata kwenye tarafa yake na kuiwasilisha kwa Mkuu wa Wilaya.
• Kuhamasisha na kuhimiza wananchi iliwashiriki kwenye shughuli za maendeleo kwenye Tarafa.
• Kuwa kiungo kati ya Serikali kuu na Wananchi Katika Tarafa.
• Kuwa mlinzi wa amani katika eneo lake.
• Kufuatilia na kuhimiza utekelezaji wa sera za Serikali katika eneo lake na kuhakikisha kuwa zinatekelezwa ipasavyo.
• Kuratibu shughuli zote za maafa na dharura mbalimbali katika eneo lake
• Kuandaa taarifa zote zinazohusu masuala ya Serikali Kuu kuhusu utendaji wa kazi za maafisa Watendaji wa kata wa eneo lake na kuziwasilisha kwa Mkuu wa Wilaya.
• Kuwa kiungo kati ya Serikali kuu na Serikali za Mitaa. katika eneo lake.
• Kufanya kazi zingine atakazopangiwa na Katibu Tawala wa Wilaya.
(ii) Kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa;
• Kuwasaidia Wakurugenzi wa Serikali za Mitaa katika shughuli za Maendeleo katika eneo lake
• Kusimamia utendaji wa shughuli za Maafisa Watendaji wa Vijiji, Kata na Mitaa.
• Kushiriki na kutoa ushauri katika upangaji wa mipango ya Maendeleo katika eneo lake
• Kuhudhuria vikao vya kamati za Halmashauri na Baraza la madiwani na kutoa ushauri.
• Kuandaa taarifa za utekelezaji wa kazi katika eneo lake kama zitakavyopokelewa kutoka kwa Watendaji wa Kata.
• Kusimamia utekelezaji wa Sheria ndogondogo za Halmashauri ya Wilaya, Miji, Manispaa au Jiji.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom