KCB yatoa sh 325M kudhamini ligi kuu Vodacom

kirerenya

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2013
Posts
1,696
Reaction score
2,253

Benki ya KCB Tanzania leo imetangaza rasmi udhamini mwenza wa ligi ya soka ya TFF Vodacom 2017/18 wenye thamani ya shilingi za kitanzania 325,000,000. Mkataba wa makubaliano hayo ulisainiwa rasmi leo na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya KCB Cosmas Kimario na Raisi WA TFF Wallace Karia.

Hafla hiyo ya makubaliano ilihudhuriwa pia na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Benki ya KCB Tanzania, Bi, Zuhura Muro, Mwenyekiti wa bodi ya Udhamini TFF, Mhe, Mohammed Abdulaziz, Wakurugenzi wa Bodi ya KCB Tanzania, Wafanyakazi Benki ya KCB Tanzania, wawakilishi wa vilabu vinavyoshiriki ligi kuu ya soka na waandishi wa habari.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kusainiwa mkataba huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya KCB Cosmas Kimario alisema kuwa udhamini huo upo ndani ya vipaumbele vya benki kuleta maendeleo katika sekta mbalimbali za kijamii ikiwemo michezo. “Sekta ya michezo ina mchango mkubwa katika kuleta maendeleo ya kiuchumi na kijamii na pia ni chanzo cha ajira kwa vijana wengi nchini, hivyo benki ya KCB imechukua uamuzi huu kujiunga na TFF kukuza mchezo wa mpira wa miguu” alisema Kimario.

Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya KCB Tanzania Zuhuru Muro alisema kuwa “Benki ya KCB Tanzania tunajivunia kuwa sehemu ya ligi hii na tunaamini kuwa udhamini wetu utachangia kuleta hamasa kubwa kwa wapenzi wa mpira wa miguu na kukuza vipaji vya vijana.” Alieleza kuwa udhamini huo utakuwa chachu ya maendeleo kwa benki, wateja wake, TFF, wachezaji, mashabiki na wananchi kwa ujumla.

Rais wa TFF aliishukuru benki ya KCB kwa kuidhamini Ligi kuu Vodacom jambo ambalo alisema litasaidia kufanikisha msimu huu wa ligi kuu 2017/18. Pia alizitaka taasisi zingine na watu binafsi kuiga mfano huo kuweza kutoa michango ya hali na mali ili kukuza maendeleo ya soka kwa timu za ligi kuu.

Chanzo: Michuzijr

 
325M ni pesa nyingi sanaaaa ila kwa thamani sahihi ya ligi yetu hiyo pesa ni mwendelezo wa dharau ya wadhamini kwa ligi yetu.
 
ligi tunayotarajia kuwa team 20 hiyo hela itasaidia nn
 
Tatizo ni umaskini wa Mali na kujitambua.
Hiyo hela ni nyingi lakni kwa ligi nzima mhhh
Hao wangeshauriwa waidhamini MBAO FC.
 
Waache ujinga wa kuchezea mpira.

Diamond ana Honga 500000 kwa wiki.

Afu timu 16 za wachezaji 30@ unaipa 300M b4 upigaji?

Huu ni uenda wazimu nchini!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…