KCMC waamua kuua sasa!

Eeka Mangi

JF-Expert Member
Joined
Jul 27, 2008
Posts
3,173
Reaction score
482
Taarifa za uhakika toka chanzo cha uhakika ndani ya KCMC zinasema kuwagharama za matibabu zimepanda. Kupata kitanda tu bila hata panadol ni shiling 35000/- a very minor surgery ni kuanzia laki mbili kwenda juu. Boda boda mkae mkijua kuwa sasa ukivunjika mguu ni 1,500,000/-
Msamaria mwema bwana!
 
unaandika habari unarukaruka ,tulia,jipange.kwani wameua nani,hakuna tiba ya bure mkuu,ww ulitaka bure? halafu ww umeishia darasa la ngapi? utoto ndani ya jukwaa hatutaki.
 
Ni kweli hizi bei ni kubwa.
Lakini mbona mnailaumu KCMC kana kwamba wao ndiyo wenye kauli ya mwisho kuhusu maisha ya watanzania?
udhaifu huu mama yake ni serikali ya CCM. Serikali makini haiwezi kunyamaza kimya wakati tune ya huduma muhimu za wananchi wake inapanda juu kiasi kwamba watu wote wa kawaida hawataweza kuzimudu.

Ninapeleka lawama zangu zote bila ajizi wala hofu kwa serikali nikiwa nimejiaminisha kwamba sasa kazi ya serikali yetu ni kukusanya kodi kutoka kwa wanyonge na kuzitumia fedha hizo bila kuwafaidisha wanyonge hao.

kazi ya viongozi wetu ni kufanya matanuzi makubwa kwa gharama ya maisha ya walalahoi.

Ilaaniwe CCM siku zote!!
 
unaandika habari unarukaruka ,tulia,jipange.kwani wameua nani,hakuna tiba ya bure mkuu,ww ulitaka bure? halafu ww umeishia darasa la ngapi? utoto ndani ya jukwaa hatutaki.

Mbona mapovu yanakutoka! We unafikiri ni watanzania wangapi wenye uwezo wa kulipia gharama hizo. Darasa langu nimeishia vidudu! Kwani wewe sio mtoto ama huna wazazi! Shame on you!
 
Pitia tena tarakimu, ni 1500,00 au ni 150,000?
 
unaandika habari unarukaruka ,tulia,jipange.kwani wameua nani,hakuna tiba ya bure mkuu,ww ulitaka bure? halafu ww umeishia darasa la ngapi? utoto ndani ya jukwaa hatutaki.

Hayo maneno yenye red ndio ya kitoto na alieandika ndio atakuwa mtoto, full stop
 
Mmh kuna kitu si bure! Mbona uzi za kuiponda KCMC haziishi siku hizi humu ndani.

tragedy of the commons
 
Samahani hiyo ni shilingi ngapi vile.! mimi hesabu zimepita kushoto.
 
Ni kweli mkuu gharama hizi zilipandishwa rasmi tar 1 june 2013.
Na wakasema kama mtu huziwezi chapa lapa katafute hospitali ya babaako.
 
By THE GREAT CAMP
Samahani hiyo ni shilingi ngapi vile.! mimi hesabu zimepita kushoto.
Hiyo ni buku jero mkuu na shing sifuri
Ahsante...kweli elimu haina mwisho. Nimeipenda hiyo.
 
hiyo elfu 35000 ni kwa siku au kwa kipindi chote utakacholazwa?
 
Mmh kuna kitu si bure! Mbona uzi za kuiponda KCMC haziishi siku hizi humu ndani.

tragedy of the commons
Sio tunaponda ila kwa gharama hizi tunategemea nini mkuu! Kweli unategemea mlalahoi aweze kulipia gharama hizi?
 
Sio tunaponda ila kwa gharama hizi tunategemea nini mkuu! Kweli unategemea mlalahoi aweze kulipia gharama hizi?
Ni kweli mkuu. Lakini tatizo la gharama limekuepo hospitali mbalimbali kwasasa. mfano; Agha Khan siku hizi hawachukui bima ya afya NHIF, bima yenye idadi kubwa ya watanzania wa vipato vya chini ambao wanaweza kufika hapo kwa mgongo wa bima tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…