SoC04 Keki ya Tanzania miaka 5-25 ijayo/udhibiti wa rasilimali fedha

SoC04 Keki ya Tanzania miaka 5-25 ijayo/udhibiti wa rasilimali fedha

Tanzania Tuitakayo competition threads

Ranking1

New Member
Joined
Jun 18, 2024
Posts
1
Reaction score
0
THE STORY OF CHANGE
TANZANIA YANGU MIAKA 5-25 IJAYO (UDHIBITI WA RASILIMALI FEDHA YA WANANCHI)

Tanzania ni nchi nzuri sana iliyo na watu wazuri na imesheheni rasilimali na utajiri mwingi lakini, Tanzania hiyo hiyo imekosa mifumo sahihi ya kumeneji, kutawala na kutumia rasilimali na utajiri iliyonayo kunufaisha wananchi wake. Tanzania niitakayo ni ile ambayo, itampunguzia Rais madaraka ili afanye kazi zake kwa ufanisi zaidi. Kati ya madaraka ambayo anatakiwa kupunguziwa mojawapo ni madaraka ya teuzi. Rais ateuwe baraza lake la mawaziri tu. Teuzi zingine kama za wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya awaachie mawaziri. Nafasi ya unaibu waziri ifutwe ili kunusuru rasilimali fedha zinazotumika katika nafasi hiyo.

Tanzania niipendayo ni ile ambayo itaweka kikomo cha misafara ya Rais nje ya nchi. Rais apewe misafara 5 tu ndani ya utawala wake wa miaka 5 na kama ataongeza miaka mingine 5 basi misafara 5 mingine iongezeke. Na katika msafara huo asiende na watu zaidi ya 5. Hii ni kudhibiti rasilimali fedha ambazo zitaelekezwa katika maendeleo ya nchi.

Tanzania niipendayo ni ile ambayo itaweka kikomo kwenye mikopo ya nchi. Tanzania iwe na kikomo cha kukopa mikopo kwa maendeleo ya nchi. Athari za mikopo ni kubwa hasa nchi kulazimishwa kutoa sehemu ya utajiri wake ili kulipa deni, kulazimishwa kusaini mikataba ambayo inahatarisha nchi kwa ujumla kiuchumi.

Napenda kuona Tanzania inayowajibisha watumishi wa Serikali wanapofanya ubadhilifu wa fedha ya UMMA. Fedha za UMMA zilizofanyiwa ubadhilifu na watumishi wa serikali kwa mujibu wa ripoti ya CAG zirejeshwe zikatumike katika maendeleo ya jamii. Watumishi waliofanya ubadhilifu aidha wafilisiwe au wakatwe katika mishahara yao.

Tanzania niipendayo ni ile itakayoondoa viti maalum kunusuru rasilimali fedha inayotumika katika nafasi hizo. Mbadala wake ni kubana vyama vya siasa kusimamisha jinsi ya kike katika majimbo yao. Mfano kwa miaka mitano kama chama kilisimamisha mwanaume basi miaka mitano ijayo itasimamisha mwanamke. Hivyo jamii italazimika kumchagua mwanamke na mifumo dume itatokomezwa kabisa kama sio kupunguzwa.

Tanzania niipendayo mimi ni ile itakayopunguza mishahara ya wabunge na kuielekeza katika maendeleo ya jamii. Ubunge uwe kama kazi zingine za utumishi wa umma ili kuondoa sintofahamu za wagombea kuuana, kurogana, kutoa kafara za albino ili kushinda uchaguzi kama inavyosadikika katika jamii. Kupata kipato kikubwa cha mishahara ya wabunge kimepelekea kuhamasisha wagombea kupambana hata kuhatarisha Amani yao binafsi na nchi kwa ujumla kwa maslahi binafsi.

Ndani ya miaka 25 ijayo napenda kuona Tanzania ya kijani yenye viwanda na wananchi walioneemeshwa na rasilimali za nchi yao. Narudi kuungana na sera ya “Kilimo kwanza”, ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa awamu ya nne baba yangu Jakaya Mrisho Kikwete. Itakayowafanya vijana na wananchi kwa ujumla kufanya kazi na kujiajiri mashambani kama tu fedha zilizodhibitiwa zitaelekezwa huko. Tanzania ni kubwa ardhi kubwa sana fedha ikusanywe wasioajiriwa waingie kazini wazalishe kwa kilimo cha umwagiliaji. Visima vichimbwe kilimo kianze, viwanda vidogo vidogo vijengwe tumuone Hayati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baba Joseph Pombe Magufuli na sera yake ya Tanzania ya viwanda. Ninahitaji kuona Tanzania ya maendeleo ya mtu mmoja mmoja yanayoleta maendeleo ya nchi.

Natamani kuona wananchi wanalipa kodi na kusapoti maendeleo ya nchi yao. Natamani kuona wananchi wanawajibika kwa kutii sheria za nchi bila shuruti. Kutokana na taarifa za TRA walipa kodi ni wachache ukilinganisha na idadiya wananchi wanaotakiwa kulipa kodi. Hii ni kwasababu wengi wao hawana shughuli za kufanya au, walio nashughuli za kufanya hawalipi kodi kutokana na kukata tamaa na serikali yao kwa kukosa huduma stahilki katika jamii.

Swala la ajira linageuka kuwa janga la Taifa sasa. Kila mwaka vyuo vinamwaga mtaani wahitimu lakini wengi wao wanakuwa hawana kazi. Napenda kuona Tanzania inayowajibika kwa watu wake ipasavyo. Picha niionayo leo katika ajira za vijana ni kwamba vijana wamekuwa kama watoto yatima kwa serikali yao. Nguvu kazi ya Taifa imelala. Hawa vijana wangeweza kutengenezewa mazingira wakazalisha mashambani, wakapelekwa katika sekta ya madini wakazalisha kule hakika Tanzania yetu ndani ya miaka 25 itakuwa ya kijani na yenye maendeleo makubwa.

Hotuba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Utekelezaji Mh.Prof. Kitila Mkumbo iliyosomwa Bungeni iliyonyesha jinsi gani sekta ya kilimo ilivyoingizia nchi kipato na kupelekea Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuipa kipaumbele sekta hiyo kwa bajeti ijayo. Napenda kuona Tanzania jumuishi katika ulaji wa keki ya Taifa. Tanzania ambayo wote, Serikali na watu wake wanawajibika kila mtu katika sehemu yake. Tanzania yenye watu wasio na ubihtnafsi wa kushibisha matumbo yao tu. Tanzania yenye watu waadilifu na wazalendo. Tanzania ambayo kila mwenye nacho anamshika mkono asiyenacho na kumwinua. Tanzania ya watanzania wenye kuwajibika na kuipenda Serikali na viongozi wao.​
 
Upvote 4
Back
Top Bottom