Kelele kuhusu Kocha mpya Simba hazitoshi

Mbigirikavu

Senior Member
Joined
Aug 19, 2022
Posts
101
Reaction score
118
Salaam,

Mgunda hapewi mkataba, wala kocha mpya haletwi, na uongozi hausemi chochote. Tunajua kwamba Mgunda alikuja simba kwa dharura ya kusimamia timu kwenye mashindano ya kimataifa, hasa mechi ya Simba dhidi ya Nyasa Big Bullet tu. Hata ile ya Angola de Agosto haikufikiriwa kama Mgunda angekuwepo kabla hajapatikana kocha mpya.

Kutokana na timu kufanya vizuri, wadau mbalimbali walishauri Mgunda apewe mkataba lakini uongozi umegoma kumpa, na kugomea kuleta kocha mwingine hadi leo.

Kwa bahati nzuri sasa mafuta yameshajitenga na maji. Imeshafahamika kuwa ni utaratibu wa wachezaji kucheza vizuri na kujituma anapokuja kocha mpya ili kuwania namba. Kocha akishapata kikosi cha kwanza tu wachezaji hurudi katika maisha yao ya kawaida.

Kwa sasa wachezaji wengi wa Simba wanashuka viwango kwa sababu mgunda anatumia vipaji vyao binafsi, hakuna nyongeza ya ujuzi kutoka kwa kocha, mwisho wake ni mbaya.

Yaani mchezaji kama Akpan ametokea Coast pamoja Mgunda, na alikuwa akimtumia kila mechi, leo wote wako Simba na hachezeshwi, inashangaza! Phiri na Kibu, Phiri ni bora sana kwenye kufunga, lakini mipira mingi ya kumalizia inamfikia Kibu badala ya Phiri, hapo lazima kuna shida tu.

Huu ndiyo muda muafaka kuleta kocha ambae ana uwezo wa kukuza vipaji. Awasaidie wachezaji kuongeza taaluma yao ya mpira. Aletwe kocha sasa hivi, ili akae na kikosi kabla mashindano ya kimataifa hayajaanza Februari.

Siwaamini sana viongozi wa Simba, wakiachwa hivi hivi wanajiborongea mambo. Lazima wapigiwe kelele ndiyo wanajishughulisha. Na sisi mashabiki tusisubiri mambo yaharibike, mwelekeo umeshaonekana. Tuwapigie kele viongozi. Kelele kuhusu kocha mpya.
 
Yamekuwa ayo tena, pira si linatembea na mgunda anatosha na atawavusha kocha wa kigeni wa nini🤣🤣🤣
 
Tulisha waaambia achaneni na Yanga na nyinyi Simba mna mechi zenu hamkutaka kusikia Sasa yamewakuta, kinacho fuatia mtasema Yanga ana nunua mechi.[emoji1][emoji1][emoji1]
 
Kuna shabiki mmoja anaitwa Kalpana, humwambii kitu kuhusu Guardiola mnene! Yaani siku ya kutimuliwa Kocha Juma Mgunda, nahisi atalia sana kwa huzuni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…