Yussufhaji
Member
- Sep 9, 2018
- 35
- 28
KELELE ZA CHINA DHIDI YA NCHI ZA NJE KUINGILIA UCHAGUZI WA TANZANIA SIO KELELE ZA CHURA MTONI!
Taarifa ya China iliyotolewa na msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya nchi hiyo bwana Zhao Lijian kuhusiana na imani ya China juu ya kutambua uwezo wa Tanzania kusimamia kwa ufanisi uchaguzi wake na kuzitaka nchi nyengine kuacha kuingilia uchaguzi mkuu wa Tanzania naotarajiwa kufanyika Oktoba 28 sio kelele za chura mtoni!
Kelele hizi kwa maoni ya Mtoto wa Mkulima zinachagizwa na shughuli na taarifa mbalimbali zinazotolewa na nchi nyengine mfano Marekani kuhusiana na uchaguzi mkuu wa Tanzania.
Bila ya shaka Mbiu ya mgambo, ikilia kuna jambo! Naweza kuthubutu kusema pamoja na shughuli na taarifa mbalimbali zinazotolewa na nchi za nje juu ya uchaguzi wa Tanzania, zipo sababu nyingi zinazochagiza kutolewa kwa tamko hilo kutoka China, ikiwemo kutaka kuudhihirisha umma utayari wa China kuiunga mkono Tanzania kwa lolote lile linalohusiana na uchaguzi unaoendelea katika uwanja wa kimataifa na kuonesha uswahiba wa dhati na urafiki uliopo baina ya China na Tanzania ambao umechagizwa na matukio mbalimbali ya kihistoria.
Yawezekana pia China inajihisi kuwepo kwa kitisho cha maslahi yake mbalimbali nchini Tanzania kwa kadri ushawishi wamataifa mengine unavyoengezeka, takwimu mbalimbali zinaonesha hadi kufikia mwaka 2018 China ndio mshirika wa kwanza wa kibiashara wa Tanzania katika uagizaji wa bidhaaa na uwekezaji ambapo katika uagizaji wa bidhaa, bidhaa zenye thamani ya USD 1.77 bilioni ziliagizwa kutoka China katika uwekezaji ikiwa ni USD 177.5 milioni huku China na Tanzania kwa kushirikiana na Oman zikiwa na mradi mkubwa wa pamoja wa ujenzi wa bandari ya kisasa katika mji wa kale wa Bagamoyo wenye thamani ya USD 19 bilioni ambapo pamekuwa na mazungumzo kedekede kuhusiana na mradi huo.
Unaweza pia kuthubutu kusema vita baridi iliopo baina ya China na Marekani imechagiza pia kutolewa kwa tamko hilo la China ambapo nchi hizo zimekuwa zikichuana nguzu za kijeshi na kiuchumi, kwa mujibu wa takwimu za shirika la fedha duniani IMF zinaonesha Marekani inaongoza uchumi wa dunia kwa GDP: 20.49 trilioni huku ikifuatiwa na China GDP: 13.4 trilioni huku kwa mujibu wa mtandao globalfirepower.com inaionesha Marekani ikiongoza dunia kwa nguvu za kijeshi ikifuatiwa na Urusi na China huku mtandao wa brookings.edu ukiionesha China kuwa na idadi kubwa ya wanajeshi ambayo ni sawa na mara mbili ya idadi ya wanajeshi wa Marekani.
Migogoro mengine ya kimataifa kama migogoro ya kimipaka iliyopo Asia Pasifiki, Mashambulizi na tuhuma za Rais Donald Trump dhidi ya China kuhusu ugonjwa wa covid 19, mgogoro wa Korea kusini na Kaskazini, Taiwan, Japan na Ukomunist na Ubepari yawezekana pia.
Pamoja na kuzijua sababu zilizochochea China kutoa tamko hilo, maswali mawili ya kujiuliza Je China ina haki ya kutoa tamko hilo? Ni kweli Tanzania inao Uwezo wa kusiamamia chaguzi zake kwa ufanisi?
Kwa mujibu wa sheria za kimataifa ikiwemo charter ya UN, article 2, inakataza nchi nyengine kuingilia masuala ya ndani ya nchi nyenginezo, hii inaipa haki China kukemea kama imeona viashiria hivyo kama tamko lake linavyojieleza, vilevile China ni miongoni mwa nchi zenye kura ya turufu (veto) katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ambapo pia ni mwanachama wa kudumu baraza hilo.
Kuhusiana na uwezo wa Tanzania kujisimamia chaguzi zake kwa ufanisi, sio suala la kutilia shaka hata kidogo kwa kuzingatia na chaguzi za nchi nyenginezo katika ukanda wa nchi za maziwa makuu, Tanzania imekuwa ikijivunia amani na utulivu wakati wote wa chaguzi zake pamoja na kuwepo kwa dosari mbalimbali, vilevile kama inavyoelezwa uchaguzi mkuu wa 2020 kwa asilimia 100 utagharamiwa na fedha za ndani.
Tamko lililotolewa pia na ubalozi wa Marekani nchini linadhihirisha uwezo wa Tanzania kujisimamia, nikinukuu
" Tanzania’s history of peaceful multi-party elections stretching back 25 years has made it a model on the continent."
Mwisho wa makala yangu hii iliyojaa maoni na fikra zangu binafsi kufuatiwa na tamko lililotolewa na China kukemea nchi za nje kuingilia wa uchaguzi wa Tanzania kwa kuwaomba wa Tanzania wenzangu tuilinde amani yetu, tujitokeze kupiga kura bila ya kupoteza haki yetu hii. Muhimu upendo, mshikamano na utulivu, tunu hizi tusizipoteze huku nikitambua dosari ndogondogo ziliopo, TUVUMILIANE!
Mawasiliano
Fb: Yussuf hajj Khatib
Email: hajjyussuf2@gmail.com
Simu: +255777158131