Victor Mlaki
JF-Expert Member
- May 1, 2016
- 4,151
- 4,277
UVUMILIVU NA USIRI WA SIS OSINACHI NWACHUKWU UNAMUONESHA MAMA WA KIAFRIKA NA KELELE ZA UKIMYA.
Mama wa Kiafrika anapitia safari iliyojaa kelele za ukimya zinazomtaka awe mstahimilivu na kikubwa zaidi awe msiri juu ya madhila yote anayoyapitia katika KIFUNGO cha staha. Siandiki kumtetea Mwanamke kwa sababu nafahamu wanaweza kujitetea wenyewe.
Msukumo uliopelekea kuandika yote haya ni masuala yaliyoibuka baada ya kifo cha Mwimbaji wa nyimbo za Injili Nchini Nigeria, Dada yetu mpendwa Osinachi Nwachukwu. Masuala hayo yameonesha picha ya Mwanamke ilivyo hata katika jamii yetu ya Kitanzania na hivyo nimejikua nikitamani kuandika ili tujifunze kwa pamoja jambo hili nililoliona.
Sis, Osinachi Nwachukwu aliweza kuwasiliana na Mchungaji Dr Paul Enenche mara nyingi na kumshirikisha mengi mno yaliyohotaji maombi. Hata alipohitaji kupelekwa hospitali aliwasiliana na mchungaji huyo lakini "YAPO ALIYOYAFICHA" licha ya Mchungaji huyo kufahamu mengi lakini yapo ambayovMchungaji alifichwa na ameyafahamu mara baada ya kifo cha Mwimbaji huyu " Siri ya Mama wa Kiafrika"
Kulingana na maelezo ya Mchungaji, Dr Paul Enenche ni kwamba yapo aliyofichwa na ndiyo haya niliyoyaita "kelele za ukimya za mwanamke".Ilibainika kuwa Mwimbaji huyu alikuwa anafanyiwa ukatili wa kijinsia mara kadhaa na mumewe lakini yeye mwenyewe hakutaka Mchungaji wake afahamu hilo (siri), mara kadhaa hata pacha wake alitaka kumshirikisha Mchungaji huyo baada ya kushuhudia ukatili lakini Mwimbaji huyo alimuomba sana asiitoe siri hiyo (kelele za ukimya).
Ekweuemee.....ekwuemee...You are the living God, Eze no one like you..ni wimbo uliofariji sana lakini ulikuwa umebeba kelele za ukimya na siri za Mama wa Kiafrika. Mama aliyediriki kulizwa na kujinyima haki ya kulia, machozi yakaingia moyoni. Kumbuka Mama huyu ni sawa kabisa na Mama yeyote wa Kiafrika, ni sawa na Mama yangu na inawezekana àkawa sawa na Mama yako kwa sababu utamaduni wa usiri umejikita kwenye mfumo jamii na jamii zetu za Kiafrika zinafanana kwelikweli.
Mwimbaji huyu alitunza siri na waliotaka kuzitoa aliwaomba wasizitoe kwa sababu aliamini kuwa Mwanamke ni siri. Na alikwenda mbali zaidi kujiridhisha kuwa siri hiyo ni yake. Siri ya uchungu, siri ya maumivu chini ya kivuli cha ustahimilivu. Maneno aliyoyasema Mch. Dr Paul Enenche kuwa "ni afadhali kuwa peke yako kuliko kuishi katika ndoa ukivumilia ulatili wa kijinsia" yanatupa taswira pana sana na mtazamo mpya wa ndoa zetu hususani sisi tunaosali makanisani na kumwamini Mungu mmoja wa kweli aliyeziumba mbingu na Nchi.