Ojuolegbha
JF-Expert Member
- Sep 6, 2020
- 1,278
- 797
TAARIFA KWA UMMA
KUKEMEA UKATILI DHIDI YA MTOTO MALIK HASHIM KITUMBI
KUKEMEA UKATILI DHIDI YA MTOTO MALIK HASHIM KITUMBIDodoma, 19, Julai, 2024
Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum pamoja na mambo mengine ina dhamana ya ulinzi na usalama wa mtoto. Wizara imepokea kwa masikitiko kitendo cha ukatili dhidi ya mtoto Malik Hashim Kitumbi mwenye umri wa miaka sita (6) aliyejeruhiwa shingoni kwa kitu chenye ncha kali tarehe 16 Julai, 2024 eneo la Goba jijini Dar es Salaam na anayedaiwa kuwa ni Msaidizi wa kazi za nyumbani (House Girl) anayefahamika kwa jina la Clemensia Cosmas.
Wizara inalaani vikali kitendo hicho kwani kililenga kukatisha/kuhatarisha uhai na maisha ya mtoto Malik Hashim Kitumbi. Wizara inashirikiana na Sekretarieti ya Mkoa wa Dar es Salaam kusimamia matibabu ya mtoto huyo ili aweze kurejea katika hali ya kawaida. Aidha, tunashirikiana na Jeshi la Polisi kumtafuta Binti Clemensia Cosmas ili aweze kufikishwa katika mkono wa sheria.
Wizara inatoa wito kwa jamii kuhakikisha inaendelea kutekeleza kikamilifu wajibu wake wa kusimamia malezi, makuzi na maendeleo ya mtoto yatakayosaidia kuimarisha ulinzi na usalama wa mtoto kama ilivyoanishwa kwenye kifungu cha 16(b) Sheria ya Mtoto Sura 13, "Kwa madhumuni ya Sheria hii, mtoto atakuwa anahitaji malezi na ulinzi endapo mtoto huyo ametelekezwa au ametendewa visivyo na mtu anayemlea na kumtunza au na mlezi wake au wazazi; ikisomwa pamoja na Kanuni za Usalama wa Mtoto za mwaka 2014 4(1) na 11(1a).
Ninawasihi Wazazi na Walezi kutumia mifumo ya huduma za Ustawi wa Jamii na mifumo mtambuka iliyopo, katika kutoa taarifa ikiwemo vitendo vya ukatili, ubakaji, ulawiti, unyanyasaji, utelekezaji pamoja na usafirishaji haramu wa binadamu.
Aidha, familia inapaswa kujua historia, anuani za makazi, taarifa za kina juu ya tabia na mienendo ya Wasaidizi wa Kazi za Nyumbani kabla ya kuwaajiri. Vilevile, Wazazi na Walezi wanapaswa kuwa na mahusiano mazuri na Wasaidizi wa Nyumbani na jamii inayoizunguka familia husika kwa