Kendrick Lamar vs Drake, nani mkali?

Singida ndio home

JF-Expert Member
Joined
Feb 23, 2012
Posts
3,188
Reaction score
3,370
Hawa watu wanafanya hiphop kweli hadi nafurahia wapo kote kwenye bars, lyrics nzuri and they do it for hiphop.

Wadau naombeni mawazo yenu nani mkali.
 
Ukitaka kutambua how Kendrick is good sikiliza ngoma moja inaitwa money tree ndo utajua Lamar ni next level
 
Mkuu Kendrick ni noma mpaka kina Nas wamemkubali,Drake ni kelele tu
Labda ungemfananisha drake na b.o.b
 
Mkuu Kendrick ni noma mpaka kina Nas wamemkubali,Drake ni kelele tu
Labda ungemfananisha drake na b.o.b

Yaani kabisaaaa Drake umlinganishe Bobby Ray?!!
K dot mwenyewe anamkubali Drake. Drake akiamua kurap ana rap kweli kweli...ni hit maker. Nas, Jay Z, Kanye, Em..wote wameshamnyooshea mikono.

Ila Kendrick nae ni mbaaaya..lyrically na kwa flow pia.

Wote hawa nawakubali..wanaishikilia new school hip hop vizuriii.
 
1.Drake ana weza kuimba na ku rap. Kendrick lamar ana rap tu.
2. Kendrick ana andika mashairi kuntu / hatari kuliko drake.
3. Drake ana fan base kubwa kuliko kendrick. Which means muziki wa kendrick mostly ni hip hop oriented which also means fans wa kendrick ni hiphop fans tena wale wanao jua maana ya hiphop kweli. Ila drake muziki wa ni flexible ana fans wa hiphop na alittle bit kama rnb hivi coz ana imba pia.
4. Kendrick ana flow style nzuri kuliko drake.
5. Drake ni mkali kwenye stage kuliko Kendrick lamar.
6. Kendrick ana funika sana aki shirikishwa kuliko akifanya ngoma peke yake. Drake ana funika hata akiwa peke yake kwenye ngoma.

Baada ya hapo nikisema nitupe kura yangu bila wasi wasi na nisije kujutia kufanya hivo hata siku na 1 nampa DRAKE. japo kua na Kendrick namuelewa sana tena sana ila kama sitaki kua disappointed hata siku 1 then DRAKE has my vote.
 

Nas Escober lini kawahi kum-nyooshea mikono Drake??
 

kwa uchambuzi wako huo, inaelekea Nyimbo za kendrick lamar unazijua 3 au 2, kwasababu huwez ukasema kendrick akifanya ngoma peke yake inakuwa DORO kuliko akishirikishwa!

Jaribu kuufatilia MUSIC vizuri!
 
kwa uchambuzi wako huo, inaelekea Nyimbo za kendrick lamar unazijua 3 au 2, kwasababu huwez ukasema kendrick akifanya ngoma peke yake inakuwa DORO kuliko akishirikishwa!

Jaribu kuufatilia MUSIC vizuri!

Naongelea hit mzee, nina nyimbo zote za kendrick lamar simjui kendrick kutoka vijiweni namjua coz namsikiliza na nina download ngoma zake, tunacho fanya hapa ni kila mtu kutoa nani mkali kwa mtazamo wake. So siwezi kusema eti kendrick kwa sababu na wewe umesema! Una sababu zako zaku mfanya kendrick awe mkali kwako, nina sababu zangu pia zaku mfanya drake awe mkali kwangu
 

Kwenye HIP-HOP huwa hatufananishi Ubora wa EMCEE's kwenye HITS, huwa tunafananisha ubora wa EMCEE's kwenye Message!

Mfano 2pac, BIG, Jay-Z etc, wanaHit nyingi sana katika career zao kuliko RAKIM, KRS-ONE, NAS na BDK (Big Dady Kane)..lakini Mpaka leo unapozungumzia One of the Greatest Hip-Hop Emcee's Duniani RAKIM huwa anachukua namba MOJA always, i mean wanaharakat na wachambuzi wengi wa HIP-HOP huwa wanamconsider jamaa kama ndo the most dangerous and complete EMCEE to ever live, japokuwa alikuwa na few hits and platnumz kuliko kina PAC na kina BIG..

Nas Escober is consdered to be "one of the greatest Hip-Hop lyricist" na ni album yake ya kwanza kabisa ya "illimatic" ndo ilimpa hicho cheo mpaka leo, na ni "moja kati ya 5 greatest Hip-Hop Album kuwah kutokea", lakin nambie ilikuwa na HITS ngapi? ukifananisha na Album yake ya pili ya "it was written"??? ambayo ilishika mpaka number 1 kwenye billboard?

Kendrick Lamar, hajaAim kwenye "mainstream rap" wakat Drake ni "pure mainstream"..drake anafanya biashara na ndo YMCMB wanachofanya, wanafanya music kulingana na soko la music linavyoenda.

Usitegemee Kendrick kufanya HITS nyingi, wakat muzik wake umeAim katika harakat na mafundisho, sana sana katika harakat za kuelezea changamoto za watu weusi na karaha zingine za maisha!..Ndo maana HIP-HOP heads kibao wa WEST COAST wanamuunga mkono (kina kurupt).

kwa aina ya HIP-HOP wanayofanya Hawa Watoto, Kendrick nadhan ungemweka kundi moja angalau na madogo wenzake kina A$AP ROCKY, siwez kumweka Kendrick kundi moja na kina MASTERACE au MURS coz bado hajafika level zile japokuwa ni generation moja. LAKINI ni matusi kumweka Kendrick na Drake kundi moja..ni kama unakuwa unafananisha uwezo wa T.I na mtu kama LIL WAYNE au NELLY which is BULLSHIT!

mistari kama hii katika ngoma yake kendrick lamar ya TODAY huwez kutegemea utaisikia kwenye hizi "mainstream radios"

F*ck the truth
F*ck Religion
F*ck the Government
F*ck the law
F*ck the Prisons
F*ck George Bush
F*ck Rappers who love dissin
F*ck you because you dont see my vision.

tofauti na ile mistari ya "all i need is them jordans" ya kina Drake..muweke Drake na kina Tyga, Big sean, J.cole, 2 Chainz, Wale, Meek mill etc coz wote hao ni "MAINSTREAM RAPPERS" hawana influence yoyote ile kwenye jamii inayowazunguka, coz wanachofanya wenyewe ni BUSINE$$ ambapo ni dhambi kuwafananisha na rappers ambao hawajaAim katika "Mainstream Rap"
 
kendrick lamar mkali sana i have got his Good kid M.A.A.D city album its so dope sichoki kuisikiliza
 
Ahsante sana Mkuu.
Sijutii kuwa mfuasi wa HIP -HOP
Vipi hapa nyumbani Emcee wa dzaini za Kendrick wapo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…