Kanungila Karim
JF-Expert Member
- Apr 29, 2016
- 20,743
- 25,564
Muchangi alifariki akiwa katika chumba cha wagonjwa mahututi alipokuwa amelazwa baada ya kukumbwa na kisanga hicho mjini Meru. Inadaiwa alitendewa unyama huo baada ya kwenda kumdai fedha walizokubaliana baada ya kumjengea nyumba bosi wake huyo.
Familia ya Muchangi imesikitishwa na tukio hilo kwa kile walichodai kuwa Polisi wamekaa kimya, Dada wa marehemu anayejulikana kama Regina Murugi amesema kuwa tukio hilo limeleta pigo kwenye familia.
“Kaka yangu amefanyiwa unyama huu lakini kwasababu ya hali yetu duni askari hawana msaada wowote kwetu, kaka alikuwa ndio kila kitu kwakweli ametuachia mzigo mkubwa sana”, amesema Regina.
Muchangi ameacha bili ya zaidi ya Shilingi Milioni 6 za Kitanzania katika hospitali hiyo ambazo ndugu zake wanatakiwa wazilipe, ndugu zake Muchangi wamelilalamikia jeshi la Polisi nchini humo kwa kukaa kimya juu ya tukio hilo.
Muchangi ametendewa tukio hilo mnamo Juni 13, 2018 kwenye kichwa chake katika eneo la Igembe Nchini Kenya, ambapo misumari hiyo ilitoboa fuvu la kichwa chake.