Kenya Airways yakataliwa usimamizi wa JKIA

clommys

New Member
Joined
Mar 10, 2019
Posts
4
Reaction score
5
Mamlaka ya usimamizi wa viwanja vya ndege ya Kenya (KAA) imetupilia mbali ombi la shirika la ndege la kenya (KQ) kupewa usimamizi wa viwanja vya ndege nchini humo kwa kusema shirika hilo halina fedha wala ujuzi wa kazi wanayoiomba na pia linaelemewa na madeni yanayoathiri utendaji kazi wake binafsi.

KAA iliimbia kamati ya Bunge ya usafirishaji na makazi siku ya Jumatano kua KQ haina ujuzi wa kuendesha viwanja vya ndege na kua uendeshaji wa uwanja wa ndege sio sawa na uendeshaji wa shirika la ndege

KAA ilisema pia hadi kufikia tarehe 31 march ya mwaka huu KQ inadaiwa na mamlaka hiyo ya viwanja vya ndege zaidi ya KSHs 5.4 bilioni.

meneja wa fedha wa KAA alitanabahisha kua kama ingekua ni mashirika mengine ya ndege wangekwisha simamisha huduma zake lakini waliliachia shirika hilo kwa kua tu linabeba jina la Kenya.

Mr ALEX GITARI, meneja wa fedha wa KAA aliyataja madeni mengine ya KQ kua ni kshs

1. CBA 3.1bn
2. NIC 2.1 bn
3. EQUITY BANK 5.2 BN
4. NATIONAL BANK 3.5 BN
5. COOPERATIVE BANK 3.3 BN
6. DTB KENYA 2.1 BN
7. KCB 2.1 BN

KQ imekua ikipata hasara kwa zaidi ya miaka 10 sasa hadi kufikia kushindwa kuendesha baadhi ya ndege zake na kuzitoa kwa mashirika mengine kama vile OMAN AIR NA TURKISH
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…