Kenya: Aliyedaiwa kuanguka kutoka kwenye ndege apatikana akiwa hai

Kenya: Aliyedaiwa kuanguka kutoka kwenye ndege apatikana akiwa hai

The Sheriff

JF-Expert Member
Joined
Oct 10, 2019
Posts
747
Reaction score
2,112
Nairobi, Kenya

Mwanaume anayekisiwa kuwa na umri wa zaidi ya miaka 30 aliyeanguka na kufariki dunia kutoka kwenye ndege ya Kenya Airways mjini London Uingereza amepatikana akiwa hai.

Mwanaume huyo ambaye picha ya mchoro wake ilionekana katika uchunguzi wa hivi karibuni akiwa amejificha ndani ya ndege amebainika kuwa hai, akiwa kwenye gereza la Kenya.

Mamlaka ya Magereza nchini Kenya ilimtaja mwanaume huyo kwa jina la Cedric Shivonje Isaac ambaye amekuwa akishikiliwa tangu mwezi Agosti na si Paul Manyasi, ambaye alitambuliwa katika taarifa ya Sky News.

Uchunguzi wa Shirika la habari Sky News wiki hii ulithibitisha mchoro wa sura ya mtu huyo na kutoa picha yake hadharani.

Ripoti hiyo ilionyesha sura ya mwanaume ambaye Sky News iliambiwa kuwa alifanya kazi kwenye kampuni ya usafi kwenye uwanja wa ndege na anayedaiwa kujificha kwenye eneo la chini ya gia ya ndege.

Lakini baadaye ilibainika kuwa mwanaume aliyeonekana kwenye picha hizo yuko hai na amekuwa akishikiliwa na polisi kwa kipindi cha miezi mitatu iliyopita.

Baba wa mwanaume huyo amekana kauli yake alipozungumza na mtangazaji wa Shirika la Utangazaji la BBC na sasa anasisitiza mtoto wake bado yuko hai. Awali baada ya kutolewa kwa mchoro huo, baba huyo alikiri mtoto wake amekufa.

Haijajulikana mkanganyiko huu umetokea vipi lakini wapelelezi wanajaribu kutafuta uwezekano kati ya Isaac, mtu aliye kwenye picha na Manyasi, mwanaume aliyetambuliwa kwenye ripoti.

Taarifa ya kupatikana kwa mtu huyo imezua maswali mapya kuhusu uwezo wa mamlaka za Kenya kumbaini mtu aliyeingia ndani ya ndege hiyo ikiwa miezi minne tangu alipoanguka kutoka kwenye ndege ya Kenya Airways kuelekea kwenye Uwanja wa ndege wa Heathrow jijini London.

Sky News wanasema walipata kidokezo cha kwanza kutoka kwa dereva wa teksi za Uber kwa jina Kamau aliyewajulisha kwamba yupo mfanyakazi wa kampuni ya kufanya usafi ya Colnet aliyetoweka kipindi hicho huku baadhi ya wafanyakazi walizungumzia kutoweka kwa mfanyakazi huyo.

Inaelezwa kuwa baadaye walikutana na mwanamke mfanyakazi wa Colnet ambaye hakutaka kutambuliwa aliyewaambia kwamba mwenzake kwa jina Paul Manyasi alitoweka mwishoni mwa mwezi Juni.

“Mara ya mwisho kumuona tulikuwa kazini, ghafla akatoweka, hakuna aliyejua alikoenda,” mwanamke huyo aliwaambia waandishi wa BBC.

Anasema baada ya taarifa hiyo, siku iliyofuata asubuhi kiongozi wao aliwaambia kuna aliyekuwa ametoweka lakini hawakuwa wanajua ni nani hasa na kwamba jambo hilo linafaa kuwa siri kwanza.

Mwanamke huyo aliyekuwa na picha za Paul alidai alikuwa na uhusiano naye wa miaka miwili na walikuwa na mpango wa kuoana.

Inaaminika kuwa Paul alikuwa akiishi mtaa wa Mukuru kwa Njenga pamoja na rafiki yake Patrick ambaye ndiye aliyemsaidia kupata kazi. Wawili hao wanatokea jimbo moja Kakamega.

Alipohojiwa kuhusu mkasa huo, Patrick alisema rafiki yake Paul alikuwa na ndoto ya kuondoka Kenya lakini hakuwahi kufichua alitaka kwenda wapi na ni kazi gani angeenda kuifanya.


Chanzo: Mwananchi

Pia soma:
 
Kwani mwili wa aliyedandia ndege si upo mamlaka inashindwa je kufanya kazi kumtambua?? Wanatumia mbinu za 1728 kumtambua?
--scanner kibao uwanjani
--camera za kutosha.
Kama na mwili usingepatikana je?
Kenya bhana
 
Pale Jomo Kenyatta International Airport pana mapungufu makubwa kuhusu usalama wa ndege.

Mara kadhaa nikiwa ndani ya terminal nimekaa ktk viti sehemu ya wasafiri kungojea flight zao, huangaza macho kuangalia shughuli za ujazaji mafuta, udobi, catering, upakuzi na uteremshwaji wa mizigo n.k katika ndege zilizopaki uwanjani.

Nikagundua kulinganisha na airport zingine ktk mataifa mengine, hapo JKIA Nairobi hakuna utaratibu madhubuti, maana watu kibao wafanyakazi na walinzi wenye magwanda ya jeshi bila silaha (of course kwa sababu maalum zinazoeleweka) walio 'bored' (boreka) wapo ktk eneo la maegesho ya ndege, taxing na runway wanazubaa zubaa, wakizurura na wakipiga soga bila kazi yoyote.

Siku nyingine nikiwa JKIA Nairobi ktk shuttle buses zilizopakwa rangi kama pundamilia / zebra, sijui conveyer belt ya upakuzi wa mizigo iligoma, nikaona msururu mrefu wa watu wa waliogeuzwa kuwa human chain wakifanya kazi hiyo huku wakilia wameamka na njaa, wakipiga zogo na matangazo kibao 'mzigo-usiibiwe utafungwa jela'. Walipwe fedha za kutosha kukimu angalau vitu muhimu kama chakula, mavazi na malazi

Niliwaza moyoni kunaweza kutokea 'mzamiaji' a.k.a stowaway akazamia ktk ndege yoyote na kutishia usalama wa abiria au maisha yake mwenyewe.

Mambo yote hayo unayaona hapo JKIA Nairobi live maana kuta zote ni za vioo hivyo kila kinachoendelea chini uwanjani sisi abiria tulio ndani ya terminal ghorofa ya juu tunakiona na kukifanyia uhakiki

Pia sikuona pilot au second officer wa KQ akizunguka kukagua ndege kwa nje kama ipo salama kiufundi na hakuna mtu aliyejificha ktk sehemu ya gia za magurudumu n.k hasahasa jambo hili halikufanyika kwa ndege za Kenya Airways.

Kazi kwenu KCAA KCAA | Kenya Civil Aviation Authority , Kenya Airways na KAA Contact Us > Kenya Airports Authority kutuhakikishia usalama wa mizigo, ndege na maisha ya wahudumu wa ndege na abiria wanaotumia KQ na kiwanja JKIA Nairobi na viwanja vingine ndani ya Kenya.

Hizi drama zakutafuta kufunika mapungufu kutuletea mtu aliye gerezani haziwezi kukubalika . Dawa ni kukubali mapungufu, kutoa ushirikiano, kujifunza kutokana na kosa kisha kufutilia mbali uzembe wa kiusalama.
 
Back
Top Bottom