Influenza
JF-Expert Member
- Jul 1, 2018
- 1,509
- 3,756
Baadhi ya maduka yameanza kukataa huduma ya malipo kwa njia ya simu ‘Lipa na Mpesa’ wakikwepa ada ya juu ya kuwezesha ununuzi.
Matangazo yamebandikwa madukani yakizuia Wateja kulipia huduma kwa njia ya simu yakitaja sababu ni ongezeko la gharama ya muamala kati ya simu na benki.
Wateja sasa wanahitajiwa kutoa pesa kama njia ya kulipia huduma na bidhaa. Vinginevyo, walipie kwa mfumo wa pesa taslimu.
Ilani katika moja ya maduka inasema, “Kwa sababu ya kupanda kwa gharama ya muamala kupitia simu na benki, hatutaruhusu malipo kupitia ‘paybill’ na ‘buy goods’ kutoka Oktoba 1, 2023. Tafadhali lipa kwa pesa taslimu ama utoe pesa.”
Gharama ya ada ya huduma ya pesa kupitia simu imepanda kwa sababu ya kutekelezwa kwa Sheria ya Fedha ya 2023.
Sheria hiyo ilipandisha ushuru wa bidhaa kutoka asilimia 12 hadi 15. Tukio hili lilisukuma kampuni za mawasiliano kuratibu upya ada za kuhamisha pesa kwa njia ya simu.