Kenya: Baba amuoa mwanae wa kufikia na kumuacha mkewe

Kenya: Baba amuoa mwanae wa kufikia na kumuacha mkewe

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Mwanamke mmoja aliyetambulika kwa jina moja la Grace, aliolewa zaidi ya miaka 18 iliyopita. Kama wanawake wengine, aliwaza kua na ndoa yenye Amani na furaha, lakini ndoa yake iliharibika baada ya mumewe kumuoa mtoto wao wa kwanza

Grace alipata manyanyaso mengi. Baada ya changamoto nyingi mumewe akauza mali na kumfukuza mkewe, na akajenga nyumba ya kukaa nyingine na kukaa na mkewe ambaye ni binti yao

Alipouliza kuhusu hilo, mwanaume huyo alijibu kuwa yuko huru kumuoa binti huyo kwa kuwa sib inti wa kumzaa, ni binti wa kufikia

Pia watu hao wamemfanya mtoto wa pili wa mama huyo amabye yuko kidato cha tatu kuwa teja kwa madawa waliyokuwa wanampa na kumtumia mtoto huyo kwenye kumfukuza mama yake.

kitu kilichofanya mama huyo aondoke ni kuwa kila jirani akifa mumewe huenda kulala na wajane hao, na akiulizwa humjibu kuwa ana wivu sana

mume huyo alikuwa na mahusiano na wajane na mara nyingine amekuwa akirudi na nguo au viatu vya waume zao ambazo mara nyingi vilikuwa havimtoshi.

baadae aliona risiti za hospitali ndani mwao na akagundua kuwa mumewe anatumia ARVs, alipoulizwa alimwambia naye aanze kwenda kwa madaktari ili kupata vidoknge vya kuzuia maambukizi, alipopima na kuonekana hana maambukizi aliamua kuondoka na bintiye mziwanda ambaye baba huyo alijaribu kumbaka mara kadhaa lakini hakufanikiwa.

aliondoka kwa mumewe na kuanzisha maisha yake lakini hayuko vizuri kiafya, anazimia mara kwa mara, lakini pia haja ndogo humtoka bila taarifa

hali yake ya afya inamfanya asifunge mlango wake akilala, majirani zake humfungia ili likitokea lolote usiku waweze kumsaidia.

Mtoto aliyemchukua wakati anaondoka alirudi kwa baba yake baada ya kutoridhika na hali ya maisha yao.

bint yake hivi sasa ana mtoto wa miaka mitatu, mtu ambaye anajua amezaa na mumewe

Chanzo: TUKO
 
Hii ni Africa kizazi cha wapenda ngono na ndo asili za ufukara wa watu wake!
 
Back
Top Bottom