Kenya- Babu wa Loliondo 'wetu'

Kenya- Babu wa Loliondo 'wetu'

BabuK

JF-Expert Member
Joined
Jul 30, 2008
Posts
1,845
Reaction score
329
[TABLE="align: left"]
[TR]
[TD="class: kaziBody, align: left"]BALOZI wa Kenya nchini Tanzania, Mutinda Mutiso, amesema kitendo cha nchi yake kumtangaza Mchungaji mstaafu Ambilikile Mwaisapile kuwa anapatikana
kijiji cha Samunge, Kusini mwa Kenya ni sehemu ya mbinu za biashara.

Akizungumza mjini hapa jana, Balozi Mutiso alikiri, kwamba pamoja na kutumia jina la Mchungaji Mwaisapile kuitangaza Kenya kimataifa, hakuna asiyeufahamu ukweli kwamba, kijiji cha Samunge kipo Tanzania, Loliondo Wilaya ya Ngorongoro, mkoani Arusha.

Mutiso alisema wafanyabiashara wa Kenya wana mbinu nyingi za kupata watu kutokana na
kutumia kauli za ushawishi wa kutangaza hata kama vitu hivyo havipo nchini mwao, ingawa
wakati mwingine mbinu za utangazaji huo huwa mbaya na zinaeleweka vibaya kwa nchi husika, lakini kila mtu anajua ushindani wa biashara uliopo.

Alisisitiza, kwamba Mchungaji huyo anayetoa tiba ya `Kikombe’ kwa magonjwa sugu yakiwamo kisukari, pumu, saratani na Ukimwi, yuko Tanzania na kwamba baadhi ya wakazi wa Loliondo, hutumia bidhaa za Kenya na wengine kwenda Kenya kuchukua mahitaji yao.

"Watu wanafikiri tunaharibu jina la Tanzania, lakini hakuna kitu kama hicho, huo ni ushindani
wa kibiashara," alisisitiza Balozi na kuongeza kuwa, soko la Afrika Mashariki na Jumuiya yake, vitakuwa na ushindani wa kibiashara, hivyo wananchi na kila nchi zihakikishe kuwa
wanatangaza vitu vyao kwa kila hali ili kuleta mabadiliko.

Kauli ya Balozi huyo imekuja siku chache baada ya Mbunge wa Ngorongoro, Kaika Telele, kuliambia Bunge la Tanzania kwamba Wakenya wameanza kujitangaza kimataifa, kwamba
Samunge ipo Kusini mwa nchi yao.

Telele alitoa madai hayo wiki iliyopita, alipokuwa akichangia mjadala wa hotuba ya
Makadirio ya Matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka wa fedha wa 2011/12.

“Napenda kumzungumzia Babu wa Loliondo, kwa sababu amefanya mambo makubwa sana na naishukuru Serikali kwa kumpa ushirikiano wa karibu. Nawashukuru pia wote waliokwenda Loliondo kupata ‘kikombe cha Babu’, waliopona ndio wanaojua Babu amewasaidiaje kwa sababu hiyo ni siri yao.

“Pamoja na kwamba Samunge iko Tanzania hivi sasa Wakenya wanajitangaza kwamba kijiji
hicho kiko Kusini mwa Kenya … huu si ukweli kabisa, kwa sababu wanafanya hivyo ili wageni
wanaokuja kwa Babu wapitie Kenya.

“Wanawadanganya watu kwamba, kutoka KIA hadi Samunge ni kilometa 800, wanasema
kutoka uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta hadi Nairobi ni kilometa tatu, wanasema kutoka
Nairobi hadi Samunge kupitia Loliondo ni kilometa 45 wakati usahihi ni kwamba kutoka Loliondo hadi Narok ni kilometa 156 na umbali halisi wa kutoka Narok hadi Samunge ni kilometa 200.

“Hawa Wakenya ni watu wa ajabu sana. Wanawadanganya watu kwa sababu kila kitu
kizuri kinapopatikana Tanzania, wanasema ni chao. Serengeti wanasema ni yao, Kilimanjaro
wanasema ni yao, kwa nini Serikali yetu haikanushi taarifa hizi?

“Mimi sielewi kwa nini Serikali yetu iko kimya. Wakenya sasa wanapata umaarufu wa
Samunge wakati si kijiji chao! Serikali isikae kimya, ijibu kauli hizo na iwaeleze watu ukweli
badala ya kuendelea kukaa kimya.

“Halafu mwelewe kwamba wagonjwa wengi wanaoingia Samunge wanatoka Kenya, wengi
wao si Wakenya, ni wageni kutoka nchi nyingine wanaolazimika kupitia nchi hiyo kutokana na taarifa za uongo zinazotolewa,” alilalamika Telele.

Umaarufu wa Babu wa Loliondo ulianza kuibuka mwishoni mwa mwaka jana, baada ya
kuenea kwa habari za mitishamba yake kutibu magonjwa sugu, hali iliyowafanya wagonjwa
wengi wa ndani na nje ya nchi kumiminika Samunge kwa lengo la kujipatia tiba maarufu ya
‘kikombe’.

Inakadiriwa kuwa zaidi ya watu milioni nne wameshakwenda kwa Babu hadi sasa.
Chanzo: HabariLeo

[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: Text, align: left"] [/TD]
[/TR]
[/TABLE]
 
Waache Wakenya wafaidi huu mwanya kibiashara uliotokea wakati sisi bado tunapoteza muda kubishana whether kikombe cha babu kinatibu au hakitibu. Wakenya ni aggressive kwenye biashara na wameona kuwa hiyo ni opportunity wanaitumia. Watanzania kalagha baho
 
Back
Top Bottom