Kenya bhana, kumbe hata 3000MW za Umeme hakuna!

Barbarosa

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2015
Posts
22,584
Reaction score
27,817
Huwa nasikia majigambo meengi kuhusu hii nchi, nimejaraibu kijielimisha nikagundua kwamba si lolote wala chochote, yaani jamaa hata 3000 MW za Umeme hawana, bado wako chini ya 2000 MW na hii ni nchi yenye wakazi zaidi ya milioni 40, sasa linganisha nchi ya AK inazalisha zaidi ya 40 000 MW za Umeme, na wala huwasikiii wakipiga kelele, lkn Kenya kila siku tunalishwa propaganda hapa mara sijui middle income country, mara sijui Super power wa Afrika, hivi Super power unatumia Umeme chini ya 2000 MW kwa watu zaidi ya milioni 40?

Mimi nafikiri hata huo umiddle income uko overrated for political reasons, kwa maana 2000 MW ni ndogo sana huwezi kuzalisha chochote!

Kuna kitu hakipo sawa, ...
 
Haha kijana mbona huzungumzii Tanzania kwanza maana ata uku hali si shwari

Sent from my SM-J200H using JamiiForums mobile app

Tanzania bado ni moja least developing country wakati Kenya tunaambiwa ni middle income country, sasa najiuliza wamewezaje kufikia middle income status kama nchi yenye watu zaidi ya milioni 40 hawawezi hata kutumia MW 2000 tu za Umeme? Labda kama huo Uchumi uko kwa 2% tu ya Wakenya wote vinginevyo haingii akilini!
 
Kenya iko na 2,295 MW kufikia 2017........ SA ndo mabingwa kwa umeme hapa Africa, infact south Africa alone generates over 50% of the continents electricity. Lakini hata pia hao hua wanapata blackouts nyingi kwasababu stima hii yote huenda kwa makampuni ya anglophone ya kutengeneza vyuma, magari, kuyeyusha madini n.k

Lakini ukiondoa SA hizo nchi nyengine ambazo ni middle income zoko gora moja, kwa mfano, hii hapa Nigeria, nchi ya 180Million yenye uchumi mkubwa zaidi Africa nzima

Generation capacity yao hupanda na kushuka hadi 2000MW
Nigeria's power generation drops to 2,662 megawatts - Premium Times Nigeria
 
Kenya iko na 2,295 MW kufikia 2017........ SA ndo mabingwa kwa umeme hapa Africa, infact south Africa alone generates over 50% of the continents electricity.

Lakini ukiondoa SA hizo nchi nyengine ambazo ni middle income zoko gora moja, kwa mfano, hii hapa Nigeria, nchi ya 180Million yenye uchumi mkubwa zaidi Africa nzima

Generation capacity yao hupanda na kushuka hadi 2000MW
Nigeria's power generation drops to 2,662 megawatts - Premium Times Nigeria

Ndo maana nashangaa, kuna kitu hakiko sawa, inawezekena vipi nchi ya watu karibia Milioni 200 (Nigeria) halafu iziweze kutumia hata 5000 MW za Umeme? Ninachoweza kukiona ni kwamba sehemu kubwa ya Wananchi wa hizo nchi hawamo kwenye mfumo wa Uchumi wa nchi na hivyo kupelekea labda Uchumi kuendeshwa na watu wachache tu, vinginevyo 5000 MW kwa watu milioni 200 hata kwa matumizi ya nyumbani tu hautoshi, ni mdogo mno, AK wanazalisha zaidi ya 40 000 MW na bado hautoishi wana power shortage, halafu tunaambiwa Nigeria ni Africa's biggest economy, with 5000 MW, how???
 
Kenya iko na 2,295 MW kufikia 2017........ SA ndo mabingwa kwa umeme hapa Africa, infact south Africa alone generates over 50% of the continents electricity. Lakini hata pia hao hua wanapata blackouts nyingi kwasababu stima hii yote huenda kwa makampuni ya anglophone ya kutengeneza vyuma, magari, kuyeyusha madini n.k

Lakini ukiondoa SA hizo nchi nyengine ambazo ni middle income zoko gora moja, kwa mfano, hii hapa Nigeria, nchi ya 180Million yenye uchumi mkubwa zaidi Africa nzima

Generation capacity yao hupanda na kushuka hadi 2000MW
Nigeria's power generation drops to 2,662 megawatts - Premium Times Nigeria
Dah, Jamaa umenichosha,
Nigeria wana GDP ya 525bn, wako 180ml
Halafu megawatts ngapi? 2600?? Seriously?
Nigeria is a joke of The Universe.
 
Ndo maana nashangaa, kuna kitu hakiko sawa, inawezekena vipi nchi ya watu karibia Milioni 200 (Nigeria) halafu iziweze kutumia hata 5000 MW za Umeme? Ninachoweza kukiona ni kwamba sehemu kubwa ya Wananchi wa hizo nchi hawamo kwenye mfumo wa Uchumi wa nchi na hivyo kupelekea labda Uchumi kuendeshwa na watu wachache tu, vinginevyo 5000 MW kwa watu milioni 200 hata kwa matumizi ya nyumbani tu hautoshi, ni mdogo mno, AK wanazalisha zaidi ya 40 000 MW na bado hautoishi wana power shortage, halafu tunaambiwa Nigeria ni Africa's biggest economy, with 5000 MW, how???
Mtihani si kuzalisha umeme tu, mtihani ni viwanda vya kutumia umeme, Demand and Supply. plant ya umeme haiwezi jengwa kama hakuna demand, na pia kwa upande mwengine, mwekezaji hawezi wekeza kiwanda kama stima haitoshi, ndio maana unaona kila siku tunaskia campuni ya magari imejenga assembly plant lakini bado hatujawahi skia kampuni imejenga manufacturing plant sababu huku umeme hautoshi na bado supply chains za malighafi ni duni, ile siku tutatatua shida ya supply chains ya malighafi ndo utaanza kuona viwanda vya nguvu alafu hapo ndo utaona nchi zetu zikizidi kutumia umeme zaidi, kila tukiongeza 1000MW unaambiwa hio haitoshi, ongeza nyengine, lakini kwa sasa ukiongeza umeme mwingi kwa mpigo unaanza kulaumiwa...
 
Ndo maana nashangaa, kuna kitu hakiko sawa, inawezekena vipi nchi ya watu karibia Milioni 200 (Nigeria) halafu iziweze kutumia hata 5000 MW za Umeme? Ninachoweza kukiona ni kwamba sehemu kubwa ya Wananchi wa hizo nchi hawamo kwenye mfumo wa Uchumi wa nchi na hivyo kupelekea labda Uchumi kuendeshwa na watu wachache tu, vinginevyo 5000 MW kwa watu milioni 200 hata kwa matumizi ya nyumbani tu hautoshi, ni mdogo mno, AK wanazalisha zaidi ya 40 000 MW na bado hautoishi wana power shortage, halafu tunaambiwa Nigeria ni Africa's biggest economy, with 5000 MW, how???

Africa Kusini pamoja na kua na umeme wa MW 40 000 mwingi ni wakuendeshea viwanda, ila umeme unazingua na sometimes ni mgao, Maji pia ni shida sometimes maji yanaweza katika days. Nigeria, ni nchi yenye wananchi wenye KELELE kama Wakenya akati hali halisi ni UHARO wa MAISHA karibia wananchi wote. Nigeria ni watumiaji wa wakubwa sana wa Majenereta kwakua swala umeme ni kama na MVUA na JANGWA.

Ila Kenya wananchi ni masikini sana na hali ya maisha ni choka mbaya. Chakula cha hovyo hovyo kama UGALI bado ni ANASA na wengi huishi kwenye MADEBE kama NJIWA.
 
Huwa nasikia majigambo meengi kuhusu hii nchi, nimejaraibu kijielimisha nikagundua kwamba si lolote wala chochote, yaani jamaa hata 3000 MW za Umeme hawana, bado wako chini ya 2000 MW na hii ni nchi yenye wakazi zaidi ya milioni 40, sasa linganisha nchi ya AK inazalisha zaidi ya 40 000 MW za Umeme, na wala huwasikiii wakipiga kelele, lkn Kenya kila siku tunalishwa propaganda hapa mara sijui middle income country, mara sijui Super power wa Afrika, hivi Super power unatumia Umeme chini ya 2000 MW kwa watu zaidi ya milioni 40?

Mimi nafikiri hata huo umiddle income uko overrated for political reasons, kwa maana 2000 MW ni ndogo sana huwezi kuzalisha chochote!

Kuna kitu hakipo sawa, ...

Huwezi zalisha alafu ukose mnunuzi.
Industrialization lazima ikue hand in hand na uzalishaji wa umeme.
But there are plans to grow the production considerably by 2025. Actually the plan was to get to 5000 by 2022 if I remember right.
 
Hawana lakini wana akili na mipango....

Embu elezea hiyo akili yao mipango, kwa maana kama watu milioni 40 hawafikishi 2000 MW, sielewi hiyo mipango unayoiongelea, kwani bila umeme huwezi kufanya chochote Dunia hii!
 
Huwezi zalisha alafu ukose mnunuzi.
Industrialization lazima ikue hand in hand na uzalishaji wa umeme.
But there are plans to grow the production considerably by 2025. Actually the plan was to get to 5000 by 2022 if I remember right.

Sidhani, nafikiri Umeme unapaswa uwepo kwanza ndiyo uzalishaji uje, na siyo kinyume chake, Umeme ni chachu ya Industrialization, kwanza ukiniuliza mimi ningeshauri hata nchi zetu ziache kila kitu na tuwekeze kwenye Umeme tu hata kwa kipindi chote cha miaka 5, ili tuwe na kuanzia 20 000 MW huko ndiyo sasa tuanze mipango mingine!
 
Ndo maana nashangaa, kuna kitu hakiko sawa, inawezekena vipi nchi ya watu karibia Milioni 200 (Nigeria) halafu iziweze kutumia hata 5000 MW za Umeme? Ninachoweza kukiona ni kwamba sehemu kubwa ya Wananchi wa hizo nchi hawamo kwenye mfumo wa Uchumi wa nchi na hivyo kupelekea labda Uchumi kuendeshwa na watu wachache tu, vinginevyo 5000 MW kwa watu milioni 200 hata kwa matumizi ya nyumbani tu hautoshi, ni mdogo mno, AK wanazalisha zaidi ya 40 000 MW na bado hautoishi wana power shortage, halafu tunaambiwa Nigeria ni Africa's biggest economy, with 5000 MW, how???
Mambo ya uchumi ni simple sana. Advice naeza kupea ni enda Wikipedia search how to calculate GDP. Au kama unaeza access library ya chuo kikuu pia enda utafute kitabu ya uchumi haswa Macroeconomics na usome how to calculate GDP. Lakini kwa ufupi GDP ni mali yote iliyopo kwenye nchi fulani. Unaangalia thamani ya majengo yote kwenye nchi hiyo. Kenya ina the biggest real estate sector in EA. Kisha Unaangalia thamani ya manufacturing sector. Kenya ina one of the biggest manufacturing sectors in E.A . Hatuangalii power generation bali size of manufacturing sector. Kisha tunaangalia thamani ya Agricultural sector (which is 30%) of KE GDP. Sector zingine ni mining, service, infrastructure and so on. Ukijumulisha haya yote utapata KE ina GDP ya $70 bn as of 2017. Hata kama electricity generation ni 2, 300 MW. sisi hatuna industry kubwa kama AK lakini tuna mali kushinda kila nchi hapa EA. Soma Mambo ya GDP and how to calculate it, hata si ngumu kuelewa
 
Embu elezea hiyo akili yao mipango, kwa maana kama watu milioni 40 hawafikishi 2000 MW, sielewi hiyo mipango unayoiongelea, kwani bila umeme huwezi kufanya chochote Dunia hii!
Umerekebishwa na hujirekebishi? umeambiwa mara kadhaa kwamba ni 2, 300 MW sasa kama unataka kuamini below 2, 000 MW then hausaidiki
 
Ndiyo maana nasema kuna kitu hakipo sawa, ni swala la kimtazamo tu, hata TZ kama tukichukua informal sector yote tukaiweka kwenye GDP yetu pia tutakuwa middle economy kama Kenya, ndiyo maana binafsi siko sana kwenye mambo ya GDP kwa maana inategemeana na mambo mengi, lkn hili la matumizi Umeme ndiyo kwangu mimi ndiyo linalotoa hasa jibu la nchi imeendelea kwa kiasi gani, hivyo kutumia chini 3000 MW kwenye nchi yenye watu zaidi ya milioni 40 kwangu mimi ni inaonyesha jinsi gani bado ni underdeveloped people, ...
 
Umerekebishwa na hujirekebishi? umeambiwa mara kadhaa kwamba ni 2, 300 MW sasa kama unataka kuamini below 2, 000 MW then hausaidiki

OK 300 MW zaidi, nitabadilisha, lkn kwa bahati mbaya sina uwezo wa kurekebisha heading!
 
Nafikiri umejibiwa vizuri na wadau wote humu na umetuliza huo moto ulioanza nao, maana siku zote unaongelea Kenya na kujifanya kuijua nchi yetu kumbe leo ndio unaanza kuitafuta Kenya kwenye Google.

Umeme huwa unazalishwa sambamba na matumizi, huna haja uzalishe umeme halafu uwe tu bila matumizi kisa unataka uonyeshe ubabe. Hata hiyo Afrika Kusini unayoisifia, fahamu umeme wake wote huo asilimia 50% unakwenda viwandani maana wamewekeza kiviwanda.
 
Back
Top Bottom