Kuna uhusiano wa matumizi ya Umeme na GDP per capital, labda kama unasema GDP total, hapo sawa lkn GDP per capital ni kipato cha mtu mmoja mmoja kwenye nchi husika, au kwa maana nyingine ubora wa maisha wa Wananchi wa nchi husika.
Hivyo kama una GDP per capital kubwa ni lazima pia utakuwa na matumizi makubwa ya umeme, kwa mfano nilikuwa nasoma nchi ya Trinidad na Tobago, ina wakazi kama milioni 1.3 (ambapo ni ndogo kama mara 30 zaidi ya Kenya na TZ) na wanatumia 2000 MW za Umeme, na GDP per capital yao ni zaidi 15,000 USD, hivyo unaweza kuona tofauti hapo na nchi zetu, wakt sisi tuko zaidi ya milioni 40 lkn tunatumia Umeme chini ya 3000 MW, hivyo matumizi ya Umeme yanasema pia jinsi nchi xyz ilivyoendelea!