Hii ni thibitisho tosha kwamba viongozi wenu wamekua wakiwadanganya na kuwaaminisha kwamba Kenya inafanya vizuri katika mambo mengi kuliko nchi zingine. Hii ndio chanzo cha wakenya kudhani wapo mbele katika kila jambo hapa Africa, kusingekuwepo na hii teknolojia ya "mass communication" na mitandao ya Kijamii, kusingekuwepo na njia yoyote kwa wakenya kujua ukweli wa hili swala, wangebaki kuamini maneno yake.
Kuna vitu vingine vinasikitisha na kukera sana toka kwa viongozi wa Kenya, waziri wa fedha anajua ukuaji wa chumi zote za Afrika, iweje anadanganya hadharani kiasi hiki?, James Macharia baada ya kuwaletea wakenya outdated diesel railway, anawadanganya wakenya kwamba ni Chinese class one, inaonekana viongozi wa Kenya wanawadharau sana wananchi wa Kenya au wanajua kwamba wakenya ni watu wenye kupenda sifa kwahiyo lazima wazungumze mambo ambayo yatawafanya wakenya wajione wapo juu hata kama sio kweli