Kenya Election 2007: Outcomes

Kuna mtu kaniambiwa kuwa Odinga amekamatwa kwa uhaini,

kuna mwenye maelezo zaidi ya kilichotokea?

Kuna mengi yamesemwa kuhusu Odinga, mpaka sasa yanabaki kuwa tetesi. The Big News inasubiriwa saa nane alasiri hapo uhuru Park if at all tetesi zote tulizozisikia zina ukweli wowote. Let us wait and see what will happen at 2:00 PM EAT!
 
jamani tumfikishie katibu mkuu UN inteligency hii ya mauji ya halaiki kenya. Lazima hawa intelahamwe wa kenya wafikishwe ICTR kujibu mashitaka. Raila, Kibaki na Kalonzo waweke ushahidi vizuri, utu wa mwafrika hauwezi kupotea kirahisi hivi.
 
Scores dead in Kenya poll clashes


Watu wameambiwa wakitoka nje watapigwa risasi kwenye slums za karibu na Nairobi hii ni kutoka kwa BBC correspondent aliye Nairobi.
 

Kubali usikubali KIBAKA ana uchu wa madaraka sawa na M7, Mbeki na Mugabe. Kwa hizo sababu zako mbona MOI aliachia ngazi?? Kwani hakukuwa na watu behind him ambao walikuwa wanafaidi. Jamaa ni FISADI tu hao wengine ndiyo tunawasingizia.
 
Kenyan Tanzanian
I hope by grace of dead you are not shot, please feed us with the latest from the ground. Ni Kweli Raila amekamatwa?
 
Unafiki wa hawa leaders sasa UN, EU nao wako wapi?
 
Unafiki wa hawa leaders sasa UN, EU nao wako wapi?

Naamini hawa watu walikua na observers wao so nadhani wanasubiria report zao ili watoe msimamo wao.

Tusubirie
 
Naamini hawa watu walikua na observers wao so nadhani wanasubiria report zao ili watoe msimamo wao.

Tusubirie

wanasubiri report ngapi wakati Kiongozi wa EU alishatoa report yake na kasoro zote alizoziona kwenye uchaguzi. Kibaya zaidi ni kwamba ni kwamba wana mfano hai ambapo mtu wao alikuwa kwenye kituo cha kutoa matangazo ya uchaguzi wa jimbo, kura zilizotamkwa zilikuwa ni 50,000 + kidogo, na ECK wakasoma kwamba Kibaki alipata 75,000 +, a difference of 25,000 votes! Sasa wanataka report gani zaidi ya hiyo??????
 
Mtanzania,
Agenda ya ku-recount imekula mkenge, kuna news zina-flow zinasema kwamba Michuki anawatafuta ODM kwa ajili ya round table discussion ili kusiwe na vurugu nyingi. Mojawapo ya agenda za Michuki ni kuhesabu tena kura, lakini ODM wamegoma. Wanadai kwamba inawezekana wakawa wameishacheza na vyote, kuanzia masanduku mpaka na tally sheets na hivyo hawaoni sababu ya hiyo round table discussion. The only option ambayo inatolewa na ODM ni kwamba Kibaka aache ofisi kwa kukubali kwamba aliiba kura na mshindi aingie kwa haki. Bila ya hilo hakuna suluhu. (Hizi ni tetesi tu, zinahitaji verification if at all kuna mtu wa ku-confirm)!
 
K-T,
Lete updates, lakini uwe makini sana bado tunakuhitaji sana hapa JF na Mungu akulinde ili uendelee kutupatia updates of what is going on hapo Nai.
 
Kuna taarifa kuwa polisi hawajamkamata Raila, na ila wanachosema wao polisi ni kuwa mkutano wa uhuru park umezuiliwa na hawauruhusu kufanyika ......

Walioko huko please tuhabarisheni kwani viroho viko juu juu sana huku tunataka kujua kunachoendelea haswa maandalizi ya uhuru park.
 
Sasa independent media ya Kenya iko wapi? Haya yangekuwa yanatokea Tanzania media ya Kenya wangekaa kimya kama media ya Tanzania na Uganda ilivyo kimya?

Hivi hawa waandishi habari uchwara walijifunzia taalama zao wapi? Hivi Kenya walitembeza bahasha kwa waandishi wa Bongo? Au wanasubiri habari kutoka BBC, CNN na SKY news? Hizi habari wao ndio wako jikoni. Je, walituma waandishi wao wa habari Nairobi? Hao waliotumwa kama wapo wanasema nini kuhusu raia wanaopoteza maisha yao?


Isije ikawa bado wanaogopa kupigwa na mama Kibaki.
 
K-T,
Lete updates, lakini uwe makini sana bado tunakuhitaji sana hapa JF na Mungu akulinde ili uendelee kutupatia updates of what is going on hapo Nai.

Kenyan - Tanzanian huenda amekwenda kwenye maandamano au wamemkatia umeme/mawasiliano ya simu. Damn inatisha hii!
 
habari nilizozipata mpaka sasa ni kwamba,there more than 120 Kenyan who have died ,Khali ni mbaya,Ni siku ya Mapumziko ya Misiba na Majonzi Nchini kenya.ODM sasa nanae ya Mchana huu wataenda Uhuru park na wabunge wao,I dont know what will happen

Naiona Kenya kama Somalia,Ila Tanzania tumechoka kupokea Wakimbizi
 
Kenya - Tanzanian huenda amekwenda kwenye maandamano au wamemkatia umeme au mawasiliano ya simu. Damn inatisha hii!

Dua tumuombee huyu ndugu K-T maana inaonekana kuwa Polisi wameamua kufanya mauaji. Tuombe tu awe amekatiwa umeme na hayawekwa ndani au kuuawa na GSU, let us hope for the better, na akirudi atarudi kwa kishindo!
 

Nakwambia uchaguzi huu umetufundisha mengi ikiwa na ukweli kwamba hatuna media, ni utani tu ule-sio tu uwezo wa ku-analyse mambo lakini pia uduni wa technolojia ya mawasiliano. Kuna magazeti bado wanazo habari za juzi mpaka dakika hii wala hawajui kama kuna watu wanauawa huko Kenya. Halafu inaonekana hawana uwezo ku-update hizo website zao ili ku-respond na matukio yanayotokea, kwa hiyo habari za leo itabidi usiubiri kesho au keshokutwa! Tuna mengi yanayokwenda kombo TZ wakati mwingine hata hujui pakuanzia.
 
Wana JF,

Ninahisi kama Raila na viongozi wenzake watakamatwa kwa uhaini ikiwa watajiapisha. Na wakikamatwa hapo ndo mambo yatazidi kuwa balaa, maana si unajua serikali iliyoko madarakani hawatakubali hilo lifanyike.The future of Kenya is in Doldrums. Naamini mambo mengi sana yametokea tangu jana, lakini kwa sababu ya ugiza wa habari, nothing is reported. Yawezekana hata vyombo vya habari vya nje hawataki kuripoti , maana wakiripoti wanaweza kufukuzwa kutoka Kenya, si unajua tena mafisadi!
 
Jamani tumwobeeni K-T isije ikawa ameshakamatwa kwa kuihabarisha dunia kinachoendelea kenya, au amejeruhiwa???? K-T uko wapi??? coz hata haja sign out!!
120 killed??
jamani kenya, watu wanauawa, kama mmesikia yanayoendelea kisumu kwa raila, Ama kweli kibaki kaamua kuwamaliza luo, inamikumbusha kifo cha ouko waluo walikufa sana.
 
http://www.alertnet.org/thenews/newsdesk/L31404723.htm


Kenyan TV says 124 dead in election protests 31 Dec 2007 11:44:28 GMT
Source: Reuters


NAIROBI, Dec 31 (Reuters) - Nationwide riots and protests following President Mwai Kibaki's controversial re-election have killed at least 124 Kenyans, broadcaster KTN said on Monday.

After Kibaki's win on Sunday, violence erupted across the country, from the opposition heartland in the west, to Nairobi in the centre, and Kenya's Indian Ocean coast.
 
Sidhani kama huo mkutano Uhuru Park utafanyika, hadi sasa (saa Jumatatu, saa tisa alasiri) watu 124 wameshauawa, na polisi wametoa tangazo kwamba watawafyatulia risasi (na kuwauwa) watu wote watakokutwa nje ya nyumba zao jijini Nairobi.

Maafa!

Ni hali ya kusikitisha sana inayoendelea nchini Kenya. Siasa ni mchezo mbaya sana, haujali maisha ya watu wengine, ni Kura kwa ajili ya Kula, na Ushindi wa Namna Yoyote ile.

Tuwaombeee ndugu zetu waKenya, tusifunge mipaka, waTanzania hatuna jadi hiyo, wale wanokuja kwa nia ya kuokoa maisha yao waachiwe wapite... tusahau tofauti zetu na malumbano, watu wanakufa, hii ni dharura...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…