Kenya Election 2007: Outcomes

bado dakika 15 duuru la tatu...ndio mwisho...ODM WAKISHINDA WANAWEZA KUSEMA HAKUNA KUAPISHANA ...TUSUBIRI
 
Hizo ndio zake M7. Haingii Kenya kumsaidia Kibaki tu bali kuchota utajiri uliopo kenya. Lazima ataanza na sukari nk. Kumbuka alivyoingia DRC.
 
ODM usishangae wakpoteza ktk wakati huo wa mwisho.

maana huenda watu wakaahidiwa kitita kikubwa wakasaliti mambo
 
ODM usishangae wakpoteza ktk wakati huo wa mwisho.

maana huenda watu wakaahidiwa kitita kikubwa wakasaliti mambo
 
Final results:

Marende: 105
Kaparo: 101


Naomba elimu hapa.

Nadhani mshindi wa moja kwa moja inabidi apate 2/3 ya kura zote, la sivyo wanapiga mara tatu na baada ya hapo ni simple majority.

Kwa taarifa zilizopo ni kuwa ODM walishinda duru mbili za mwanzoni na sasa ni duru ya tatu.

Je, ikitokea duru ya tatu hakuna aliyepata 2/3 lakini mshindi wa duru ya tatu ikawa ni PNU, ina maana Speaker ni ODM kwa kushinda duru 2 kati ya tatu, au mshindi ni PNU kwa kushinda duru ya 3 ya mwisho?
 
Matokeo niliyoweka ni matokeo ya round ya 3. Kwa hiyo Marende ndiyo Spika wa Bunge jipya, kwa maneno mengine ODM wameshinda.

Kiungani - round ya kwanza ya pili Marende alishinda na hivyo uamuzi ukawa round ya 3 ambapo yeyote kati ya top 2 akipata kura nyingi zaidi ya mwenzake basi ndiyo anakuwa Spika wa Bunge (simple majority)!
 
Sasa M7 anatia petroli kwenye moto mkali kwa kutaraji anazima...
 
ODM pia wameshinda kiti cha Naibu Spika. Kwa hiyo ngoma yote ya Bunge iko mikononi mwa ODM. Nadhani sasa Kibaka chupi itakuwa inabana, atakuwa na shughuli pevu Bungeni na serikali haiwezi kwenda bila numbers ndani ya Bunge. Kazi iko mbele, tutaona ubabe wake kama utamsaidia!
 
hongera odm keshobyale maandamano yapo?

Maandamano yapo kama kawa .... mpaka Kibaka aachie Ikulu, maana Annan kaahirisha safari kwa madai kwamba ana flu, lakini naelewa Kibaki ana-frustrate hiyo mediation esp kama mediation itafanywa na watu makini.
 
Afadhali wameshinda na sasa watumie bunge kumnyanyasa Kibaki. Rito ana nguvu kweli kwenye kuongea, ni zaidi kabisa ya Odinga.

Nimesikia redioni walivyojibizana mwanzoni, looh! naona kulikuwa na kazi kweli kweli.

Sasa hata kamati wachukue zote, hakuna kuachiana tena.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…