Kenya: Gaidi ktk shambulio la Dustid2 atambulika, familia yake yakamatwa

As Salafiyyu91

JF-Expert Member
Joined
Jan 11, 2014
Posts
2,537
Reaction score
2,538
Maafisa wa upelelezi wanaofanya uchunguzi kuhusiana na shambulio la kigaidi la DustiD2 wameweza kumtambua mshambuliaji aliyejitolea mhanga kwa kujilipua katika eneo la 14 Riverside.

Mahir Khalid Rizik ambaye alikuwa na umri wa miaka 25 alizaliwa katika kijiji cha Majengo jijini Mombasa.

Mahir alisomea katika madrassa ya msikiti ya Musa yanayojulikana kwa sifa mbaya hasa za kuendeleza itikadi za kigaidi.

Mshukiwa alisajiliwa katika kikundi cha ugaidi kilichokuwa kikiwahangaisha maafisa wa usalama katika kijiji cha Majengo kabla ya kutorokea nchini Tanzania mwaka wa 2014.

Imeripotiwa kuwa Mahir hakuishi sana Tanzania kwani alihamia Somalia ambapo alijiunga rasmi na kikundi cha ugaidi cha al- Shabaab mwaka wa 2015.

Gaidi huyu anasemekana alirejea humu nchini kisiri kupita mpaka wa kaunti ya Mandera Jumapili Januari 13, siku mbili tu kabla ya kutekeleza shambulio la Dusit D2.

Kulingana na shahid mmoja, gaidi huyo alifika katika eneo la 14 Riverside mapema kabla ya magaidi wenzake ili kufahamu vema eneo hilo.

Kabla ya Mahir kujilipua, alikuwa akiwasiliana na gaidi mkuu Ali Salim Gichunge anayeaminika kupanga shambulio hilo kwa njia ya simu.

Kupitia kwenye kamera ya CCTV, Mahiri anaonekana akiongea kwa simu huku watu wawili wakipita kando yake kabla ya kujilipua.

Abdulahi Ogelo ambaye alimpita gaidi huyo kabla ya kujilipua aliiambia runinga ya NTV kwamba jamaa huyo alikuwa wakiwauliza wenzake mahali walikokuwa, ishara kwamba alikuwa anawaarifu aanze mashambulizi.

TAARIFA KUTOKA JESHI LA POLISI

Mke na baba mzazi wa Mahir mpaka sasa wapo chini ya ulinzi baada ya kushikiliwa na polisi kwa ajili ya upelelezi zaidi, jeshi la polisi linaamini watu wa karibu wa gaidi huyo ni muhimu sana kwa sasa ili kuweza kufahamu mizunguko yake ya mara mwisho kabla ya kutekeleza shambulio hilo.

Shambulio hilo lilisababisha vifo vya watu 21 huku kadhaa wakiachwa na majeraha mabaya ya risasa.

Kupata habari zaidi, bofya hapa: DUNDIIKA

MLIPUAJI WA KUJITOLEA MHANGA: Mahir Khalid riziki ni mzaliwa wa Mombasa - Favorite Videos

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mke na baba yake wameachiwa tyr huyu jamaa alikimbilia somalia kitambo kutoka mombasa wa nasema tareh 7 week kbla ya mashambuliz polisi walimuita mkewe kituoni na jamaa alituma hela nyingi sana kwa mkewe
 
Ndugu mimi nakukubali sana, wewe ni Muislam ns unanyesha kuchukizwa na hawa magaidi,
Sio wengine wanafurahia eti kisa wanauawa Wakristo!

Wakati magaidi hawa hawa wanauwa pia waislam wanaowaona hawana itikadi zao

Chuki za kidini zitapungua endapo wote tutaungana kupinga religious extremism ( misimamo mikali ya kidini)

Wakristo na wengine wasio Waislam pia wana wajibu wakuacha kujumuisha na kuwaona waislam wote kama magaidi au wanaunga mkono ugaidi.

Hii itaondoa chuki na mgawanyiko ambao ndio wanayotaka hawa magaidu
 
Maafisa wa upelelezi wanaofanya uchunguzi kuhusiana na shambulio la kigaidi la DustiD2 wameweza kumtambua mshambuliaji aliyejitolea mhanga kwa kujilipua katika eneo la 14 Riverside.

Mahir Khalid Rizik ambaye alikuwa na umri wa miaka 25 alizaliwa katika kijiji cha Majengo jijini Mombasa.

Mahir alisomea katika madrassa ya msikiti ya Musa yanayojulikana kwa sifa mbaya hasa za kuendeleza itikadi za kigaidi.

Mshukiwa alisajiliwa katika kikundi cha ugaidi kilichokuwa kikiwahangaisha maafisa wa usalama katika kijiji cha Majengo kabla ya kutorokea nchini Tanzania mwaka wa 2014.

Imeripotiwa kuwa Mahir hakuishi sana Tanzania kwani alihamia Somalia ambapo alijiunga rasmi na kikundi cha ugaidi cha al- Shabaab mwaka wa 2015.

Gaidi huyu anasemekana alirejea humu nchini kisiri kupita mpaka wa kaunti ya Mandera Jumapili Januari 13, siku mbili tu kabla ya kutekeleza shambulio la Dusit D2.

Kulingana na shahid mmoja, gaidi huyo alifika katika eneo la 14 Riverside mapema kabla ya magaidi wenzake ili kufahamu vema eneo hilo.

Kabla ya Mahir kujilipua, alikuwa akiwasiliana na gaidi mkuu Ali Salim Gichunge anayeaminika kupanga shambulio hilo kwa njia ya simu.

Kupitia kwenye kamera ya CCTV, Mahiri anaonekana akiongea kwa simu huku watu wawili wakipita kando yake kabla ya kujilipua.

Abdulahi Ogelo ambaye alimpita gaidi huyo kabla ya kujilipua aliiambia runinga ya NTV kwamba jamaa huyo alikuwa wakiwauliza wenzake mahali walikokuwa, ishara kwamba alikuwa anawaarifu aanze mashambulizi.

TAARIFA KUTOKA JESHI LA POLISI

Mke na baba mzazi wa Mahir mpaka sasa wapo chini ya ulinzi baada ya kushikiliwa na polisi kwa ajili ya upelelezi zaidi, jeshi la polisi linaamini watu wa karibu wa gaidi huyo ni muhimu sana kwa sasa ili kuweza kufahamu mizunguko yake ya mara mwisho kabla ya kutekeleza shambulio hilo.

Shambulio hilo lilisababisha vifo vya watu 21 huku kadhaa wakiachwa na majeraha mabaya ya risasa.

Kupata habari zaidi, bofya hapa: DUNDIIKA

MLIPUAJI WA KUJITOLEA MHANGA: Mahir Khalid riziki ni mzaliwa wa Mombasa - Favorite Videos

Sent using Jamii Forums mobile app
Ndio maisha yalivo sote tutafariki!hukumu tumuachie ALLAH

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndio inavyokuwa. Kama ana familia anahakikisha anatuma pesa za kutosha zitakazo saidia familia wkt yeye akiwa hayupo duniani

Ni Kushindwa kufikiria tu nje ya duara ya mashaka. Unaambiwa au unadanganywa kwamba tunakupatia pesa ya kutosha kwa ajili ya familia yako. Pesa ya kutosha kwa kikokotoo kipi? Pesa nyingi kwa matumizi ya wigo gani? Pesa nyingi kwa muda gani Wa kuishi hapa duniani?
 
Ndio maisha yalivo sote tutafariki!hukumu tumuachie ALLAH

Mungu Mwenye upendo wote hawezi kutuumba kwa kutuwekea complicated systems namna ile halafu kisha akataka tuwe tunajifiafia tu kama Mende au Kunguru! "Mungu" Wa namna hiyo lazima tumtilie shaka kubwa.
 
Usimuinhize mungu katika jambo la Kishetani! Mungu wetu kakataza kujiuwa au kuuwa nafsi ya mwingine

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom