Kenya hizi lugha nyingi zinafaida?

Kenya hizi lugha nyingi zinafaida?

Budaboss,unaktsia jo na izi risto za yours.Kaa hung'am sheng kula kona mzeiya,hii lugha ishavuka boda!Usimind tutakudunga kibursary ivi uingie system utoke kaa umeiva mbaya!
 
Unasema hivi kwa dhana kuwa kuna wakenya wanazungumza kiswahili tu, wengine sheng, na wale wengine kizungu.

Haikuingilii akilini ya kwamba karibu wote wana uwezo wa kuzungumza lugha zote tatu na zaidi (pamoja na lugha za asila, French, German, Chinese, Arabic nk) kwa ufasaha. Sasa hapo shida ya utangamano itatokea wapi?

Nchi kujikita katika lugha moja sio njia ua kuleta muungano. Mbona Somalia iko katika hali hii, ama zile nchi mashariki ya kati- kule uarabuni yenye misuko suko?

Kwanini mataifa mengi Uropa kama Sweden, Austria na hata Uingereza, na nchi kama India zina malugha kadhaa rasmi na bado zina muungano dhabiti ya utaifa?
Hapa Africa, nchi kama South Africa ina malugha kama kenda rasmi kikatiba, na ni taifa moja.

Kuna masuala zaidi ya lugha inayofanya nchi kuungana ama kutumbukia katika misuko suko.

Nikikuomba unipe angalau nchi moja ambayo imewahi kuingia katika virugu juu ya lugha, sidhani utapata mfano hata moja.
 
Mbona wewe hata Kiswahili chenyewe unapata tabu kukiandika? Unahitaji shule ya Kiswahili.
 
99% percent of school going children in Kenyan Cities can understand very well this post that you have wrote in swahili. Sheng' is an urban language, the same way Americans use slang. This type of languages is very common in Urban Agglomeration. Sheng' can't be taught as it usually changes over time and varies according to geographical areas. Although basic terms can be taught to those who wish to learn the language.
 
Sheng ni lugha ya zamani sana, ata wakati wa mkoloni ilikuwepo kwa hivo si lugha geni kwetu
 
Hehehe!! Wewe upo hapa unaponda lugha za Kenya, lakini Kiswahili chenyewe naona kinakupa changamoto wewe binafsi.
Hebu kampe mwalimu wako wa shule ya msingi asome ulichoandika na ulivyoandika, atalia kwa aibu. Huwa mnapenda kutuponda sisi Wakenya kwa uwezo wetu wa kuongea lugha nyingi, lakini nyie hata hiyo moja imewashinda.
 
Huo upuuzi uishie huko huko usije huku
 
Hivi kwenu maneno kama buku jero ni Kiswahili? Au mdingi n.k.
Hizo ni rejesta na misimu ambazo hutumika na kundi fulani la watu,pia yanaweza kuwa lugha rasmi pale yanapotumika mara nyingi na watu wengi mfano kuna maneno kama kasheshe ambayo yalitokea huko huko lakini muda huu ni maneno rasmi.
 
Unasema hivi kwa dhana kuwa kuna wakenya wanazungumza kiswahili tu, wengine sheng, na wale wengine kizungu.

Haikuingilii akilini ya kwamba karibu wote wana uwezo wa kuzungumza lugha zote tatu na zaidi (pamoja na lugha za asila, French, German, Chinese, Arabic nk) kwa ufasaha. Sasa hapo shida ya utangamano itatokea wapi?

Nchi kujikita katika lugha moja sio njia ua kuleta muungano. Mbona Somalia iko katika hali hii, ama zile nchi mashariki ya kati- kule uarabuni yenye misuko suko?

Kwanini mataifa mengi Uropa kama Sweden, Austria na hata Uingereza, na nchi kama India zina malugha kadhaa rasmi na bado zina muungano dhabiti ya utaifa?
Hapa Africa, nchi kama South Africa ina malugha kama kenda rasmi kikatiba, na ni taifa moja.

Kuna masuala zaidi ya lugha inayofanya nchi kuungana ama kutumbukia katika misuko suko.

Nikikuomba unipe angalau nchi moja ambayo imewahi kuingia katika virugu juu ya lugha, sidhani utapata mfano hata moja.
Kizungu ni lugha gani hiyo? Wazungu wanazungumza lugha tofauti tofauti, wengine kiingereza, kijerumani, kiitaliano, kifaransa nk. Sasa hicho kizungu sijawahi kusikia.
 
Hiyo ni misimu inakuja na kupotea kulingana na wakati.Misimu ipondani ya lugha ya kiswahili ilasema yenyewe inakujanakupotea kulingana na wakati.

Maneno kwenye lugha huwa yanabuniwa, kumbuka hata Kiswahili chenyewe kilibuniwa kwa kuchanganya maneno mengi ya Kiarabu, Kibantu na hata Kireno.
Hilo neno buku au jero linatumika Tanzania yote hadi vijijini na kwa muda mrefu, tayari limekua mbadala.
 
Watanzania tunaikataa hii lugha ya kati(English-kiswahili) ila mwisho wa siku itakuja kukolea tu.

Ni suala la muda.
 
Sina tatizo na sheng! kila lugha inakua!

Leo hii ukionana na mwingereza akaamua kuongea King's English unaweza ukaona nyota, ila maneno hayo hayo akiyaongea kwa Queen's English mnaelewana na kugonga glass
 
Umesahahu kikikuyu Mpaka naona kuna redio za Kikikuyu. Mm naona wangeitambuaa tuuu KIKIKUYU. iwe lugha yao ya Taifa. Maanaa ndo lughaa ya asil yaoo hizoo zngnee wametolewaa.
 
Back
Top Bottom