Unasema hivi kwa dhana kuwa kuna wakenya wanazungumza kiswahili tu, wengine sheng, na wale wengine kizungu.
Haikuingilii akilini ya kwamba karibu wote wana uwezo wa kuzungumza lugha zote tatu na zaidi (pamoja na lugha za asila, French, German, Chinese, Arabic nk) kwa ufasaha. Sasa hapo shida ya utangamano itatokea wapi?
Nchi kujikita katika lugha moja sio njia ua kuleta muungano. Mbona Somalia iko katika hali hii, ama zile nchi mashariki ya kati- kule uarabuni yenye misuko suko?
Kwanini mataifa mengi Uropa kama Sweden, Austria na hata Uingereza, na nchi kama India zina malugha kadhaa rasmi na bado zina muungano dhabiti ya utaifa?
Hapa Africa, nchi kama South Africa ina malugha kama kenda rasmi kikatiba, na ni taifa moja.
Kuna masuala zaidi ya lugha inayofanya nchi kuungana ama kutumbukia katika misuko suko.
Nikikuomba unipe angalau nchi moja ambayo imewahi kuingia katika virugu juu ya lugha, sidhani utapata mfano hata moja.