Kenya imebaki na wasanii makinikia

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
301,577
Reaction score
754,412
Wakati huo ikijulikana kama talented country katika uwanja mzima wa sanaa kuanzia nyimbo maigizo vichekesho mpaka kutengeneza vipindi mbalimbali Tanzania na wengineo tulikuwa nyuma kwakweli

Tusizungumzie mbali sana nyakati zile za zilipendwa ambazo mpaka leo zinahit, tuzungumzie tu miongo miwili iliyopita... Enzi za vituko mahakamani, mzee mgongoo, mama kayaii, Mwalla, Mzee Ojwang na wengine wengi waliocheza na kuvaa uhusika kamili kwenye nafasi zao

Kwenye tungo za kisasa wakaibuka kina Nyota ndogo -Nibebe, Benjamin huyu dogo aliyeimba Nchi ya kitu kidogo, bush baby? Tungo zile ziliimbika na zilikuwa na ujumbe wenye hisia

Leo hii Kenya wamebaki wabana pia, wanaojipodoa na kuvaa hereni, na kuigiza kike. Bila kuwa na ujumbe wowote wa maana.... Kweli kila zama na vitabu vyake

 
Muda ni ukuta!zama zetu sasa!bora kuchelewa kuliko kutangulia!
 
Huwa namkumbuka sana Jua Kali...ngeli ya genge.
 
Yupo pia MCA tricky the former Chokolaa...wanamwita MTU Wa chokosh...
 
Waliposhika Soko la Bongo wakabweteka, Wasanii wa Bongo walipojitambua ndo wakaanza kuwasomesha Namba hadi ss wamepoteana!
 
Kina chokoraa , kina mama kayayii, mzee ojwang, othorong'ong'o , kina karumanzira , mwala na wengineo , kwakweli walibamba sana
 
Sijui ni nini kimewakumba...

Cc MK254 Kenyan
Kwani yule wenu Joti so naye huigiza kama mwanamke, huvaa hayo mavitu hadi hata wig.

Nakubaliana na huo msemo kwamba kila zama na kitabu chake. Leo hii tunao akina Churchill
 
Tasnia ya sanaa hasa uigizaji kotekote Tanzania na Kenya imekufa. Huu utandawazi wa 'slay queens' na 'socialites' umeua kabisa sekta hiyo.

Pesa..ngono..umaarufu.
 
Pia walikuwa na Tamthilia nzuri sana ya "Tausi"ilituvutia wengi enzi hizo.na kipindi maarufu cha redio"je huu ni uungwana"?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…