Teknolojia ni Yetu sote
JF-Expert Member
- Apr 28, 2020
- 620
- 1,240
Wana sayansi toka nchi ya kenya wameweza kugundua vijidudu wadogo wadogo ambavyo vinaweza kuharibu polystyrene, plastiki yoyote kwa usaidizi wa bakteria wa tumboni.
Madaktari hao wamegundua njia hiyo ili kuweza ku control mifumo ya kudhibiti taka za plastiki kwenye jamii ya watu wa Kenya, hii ndo mara ya kwanza kwa mdudu asilia barani Afrika kupatikana akivunja vunja Plastiki na kuzila.
Timu kutoka katika kituo cha kimataifa cha physiology na Ecology ya wadudu nchini Kenya inatarajia kutenga vijidudu na vimengenywa kadhaa kuweza kuendelea shughuli ya kupunguza taka za plastiki.