Kenya imetengeneza setilaiti yake ya kwanza kabisa ambayo imepangiwa kurushwa anga za juu Machi mwaka huu.

Kenya imetengeneza setilaiti yake ya kwanza kabisa ambayo imepangiwa kurushwa anga za juu Machi mwaka huu.

mr mkiki

JF-Expert Member
Joined
Sep 22, 2016
Posts
5,588
Reaction score
11,668
Kenya imetengeneza setilaiti yake ya kwanza kabisa ambayo imepangiwa kurushwa anga za juu Machi mwaka huu.

Wahandisi kutoka chuo kikuu cha Nairobi, wakisaidiwa na maafisa kutoka shirika la anga za juu la Japan walitenengeza chombo hicho katika mradi uliogharimu zaidi ya dola milioni moja.
Setlaiti hiyo itatumika kuchunguza mienendo ya kilimo, pamoja na kuchunguza maeneo ya pwani ya taifa hilo.

Mwandishi wa BBC Tomi Oladipo anasema setilaiti hiyo ni ya umbo la mchemraba na ina ukubwa wa sentimita 10 mraba - hujulikana kama nano-setilaiti.

Japan ilitoa ufadhili na jukwaa la kuitengenezea lakini ni Wakenya wenyewe walioitengeneza.
Setlaiti hiyo itatumwa hadi Kituo cha Kimataifa cha Anga za Juu (ISS) mnamo mwezi Machi na kuzinduliwa rasmi kuizungukza dunia na roboti mwezi mmoja baadaye.

Hatua hiyo itaifanya Kenya kuwa miongoni mwa mataifa mengine saba barani Afrika yaliyo na setilaiti zinazoizunguka dunia.
Mataifa mengine ni Misri, Afrika Kusini, Morocco, Algeria, Nigeria, Mauritius na Ghana.

Kundi la wahandisi kutoka chuo kikuu cha Nairobi walioitengeza walikuwa kundi la kwanza kufaidika kutokana na mradi wa pamoja kati ya Umoja wa Mataifa na shirila la anga za juu la Japan unaolenga kuzisaidia taasisi za elimu kutoka mataifa yanayostawi kutengeneza setilaiti zao.

Chanzo: BBC
 
Tutarusha taarifa na takwimu za kupikwa kupitia kutuo chetu cha anga za juu TBC kushiriaka na ITv,Clouds ,nk
 
Tutarusha taarifa na takwimu za kupikwa kupitia kutuo chetu cha anga za juu TBC kushiriaka na ITv,Clouds ,nk
Nabii stefano alipigwa mawe
Yohana mbatizaji alikatwa kichwa
Yesu alisurubiwa
Tito anaitwa mgonjwa wa akili.
Wanadamu mtajifunza lini?
 
Ze nabii tito anazidi kutikisa nchi![emoji3]
FB_IMG_1516713535052.jpg
 
Back
Top Bottom