Inasikitisha sana wananchi wa Tanzania tunapoletewa majaribu yenye habari hewa kama hii, binafsi I would rather have uchumi ambao unachechemea kama wetu bongo, lakini unawashirikisha kimanufaa wananchi walio wengi, kuliko ule wa Kenya ambao ni Conditioned Economy, kama wa South Africa,
Yaani on the papers nchi ni tajiri sana, lakini wananchi ni masikini tena wanaolala kwenye ma-box, kule vitongoji vya Nairobi na Soweto, najua bongo tuna matatizo mengi ya kiuchumi, ila so far bado sijamuona mwananchi wa bongo anayeishi kwenye nyumba ya ma-box, infact hata mara ya mwisho nilipokuwa Rio, Brazil I was shocked kukuta hata huko nako kuna wananchi wanaoshi kwenye ma-box!
Mungu Aibariki Tanzania Yetu!
Mkuu naheshimu nondo zako daima. Na wala sistahili kukupinga..ila naomba nitofautiane na wewe hapa..
Sidhani kama hapa ulikuwa genuine NA HIYO KAULI YAKO HAPO JUU. . Umejaribu kuwa defensive lakini ukweli unabaki pale pale. Manufaa yapi hayo unayoyaongelea? you mean mwananchi wa kawaida Tanzania yuko better off, kuliko wa Kenya? au tunarudi kwenye ule wimbo wetu wa kudumu..Amani na utulivu? By all measures ziwe za UNDP, WB, IMF nk..ukweli unaujua kipato cha Mkenya na MTZ ni tofauti...
Watanzania uchumi wetu hauwezi kushindana na wakenya. Thats the bitter truth. Tunaweza kuspin kwamba uchumi wa kenya ni mkubwa lakini haunufaishi wengi, wakati sisi wa Tanzania tunajua hakika uchumi wetu infact unanufaisha wachache kuliko hata Kenya. Sasa kipi bora uwe na uchumi wa Kenya mkubwa ambao uko mikononi mwa 3% au uwe na uchumi wa kuchechemea wa Tanzania ambao vile vile umo mikononi mwa 2%?
Tanzania tuna potential kubwa sana, lakini nadhani watanzania wenzetu especially viongozi wetu ni wanafiki na walafi (greedy) kuliko wakenya. Kibaya ni kwamba wanajimask kwenye amani na upole. I am a proud African FIRST and then Tanzanian, nafurahi sana nikiona nchi ya kiafrika kama Kenya inavyopiga hatua despite madudu na rushwa kwa wachache, nafurahi ninapokuwa Paris au London nikapanda KQ as an African ni jambo la kujivunia sana ukiona mwafrika mwenzako anasonga mbele. siwezi kufurahia KLM..simply because KQ ni ya muafrika mwenzangu...personally nikiwa JKIA nikiona ile traffic ya ndege zinavyopishana..nikicompare na hapa kwetu DIA..lazima niappreciate juhudi za wenzetu maana najua..haya mambo hayakuja overnight..watu walifanya na wanafanya kazi kwa bidii!
Ile mentality ya afadhali wote tukose, mimi sina na naona ndilo jambo kubwa waafrika na watanzania tulilonalo! Kama hutimizi wajibu wako..anayetimiza wa kwake..ATAKUPITA tuu..whether you like it or not! Tanzanians can spin it the way they want..lakini hakika wakenya wanajitahidi mno! against all odds, za ukabila, chuki, rushwa, ubinafsi..wameweza kufanya makubwa kuliko sisi tunaoimba kisiwa cha amani kila siku..
Kwa hiyo kikubwa, ni kukaa chini tuangalie tulijikwaa wapi..na wala siyo tulipoangukia! Hakuna Uchumi uliokamilifu kwamba utawainua WOTE labda zile ndoto za mzee wetu Kambarage ambazo na yeye baadaye alikiri kwamba hazikuwa sahihi. Tuangalie tunaweza kushirikiana na wakenya, waganda, waburundi, warwanda wapi tuweze kuinuana..hizi nyimbo za amani na utulivu ni kudanganyana...zitakuwa na maana endapo tutazitumia kuboresha maisha ya watu wetu.
Watanzania wenzangu tuache longo longo! Hii "roho ya kwa nini" na "heri tukose wote"...tuachane nayo..haifai..tupige mzigo tuu, kitaeleweka!
Tuwaangalie wakenya kwa makini, perhaps we have one or two things we can learn from them!