Kenya imewekeza kuzipita tz and ug mbali sana.

Wakuu,

Again respect kwa huu mjadala,

Tanzania naona tunaweza kujiimarisha kila angle na kuwashika Kenya pabaya.Katika Tourism industry yenyewe,tukiwa strategic tutakua tunawapumulia kenya mgongoni.

Hili suala la kujenga viwanda vya ndani angalao ktk bajeti ya mwaka tuitenge au ni bora tungeendelea kutegemea wafadhili ktk hiyo asilimia tuliyopunguza lakini tui-invest katika kujenga hivyo viwanda.Tungeendelea kutegemea wafadhili strategically lakini tukai--invest hizo hela kwa muda wa kama miaka mitano ijayo.

Tanzania ina fursa nzuri za kujiimarisha kichumi kuliko Kenya kama tutaimarisha miundombinu.Pia tujitangaze maanake Biashara inaaendana na matangazo,hata ikiwezekana propaganda makini zitasaidia sana.Tujaribu kucheza na saikolojia za wakaazi wa dunia hii.All it's about business
 

Ulichosema ni cha busara sana. kwangu mimi ni afahali kulima kwa jembe la mkono kwenye ardhi yako kuliko kuwa nfanyakazi ukimlimia bepari kwa ujira kidogo. Je, una habari kuwa kuna kampuni moja imepewa kibali cha kuwahamisha wananchi wa vijiji kama ishirini hivi maeneo ya mkoa wa Pwani na Lindi ili kampuni hiyo ilime jatropa? Ja, wanachi hao wataenda wapi kama sio kwenda kuishi kwenye nyumba za mabox?
 

Mkuu Heshima mbele sana,

Sina uhakika na nambaz zinasema nini, lakini ninachelea nilichokiona kwenye hizi nchi, no way maisha ya wananchi wengi wa Kenya yako juu kuliko ya wa-Tanzania wengi, siwezi kuamini hayo unless kama kuna mabadiliko yametokea hivi karibuni,

I mean wananchi wanaoishi kwa kukodisha ardhi ya Kenyatta, wanakuwaje na maisha bora kuliko sisi wabongo tunaoishi kwenye ardhi za mababu zetu? Anyways nilipofika Kenya mara ya mwisho ilikuwa ni kitambo kidogo inawezekana kua maisha yalibadilika, lakini nilichokiona huko last time na ile mabasi ya Matatu, hapana mkuu I was proud to be a Tanzanian, kule Soweto na Brazil ndio kabisaa ilikuwa aibuu tupu!

Lakini bado ninaheshimu hoja zako nyingi kwenye post yako!
 
jamani nauliza,kwani life expectancy ya mtanzania ni miaka mingapi ?
life expectancy ya mkenya ni miaka mingapi? i believe hii ni a good indicator of who is who vis-a-vis maendeleo
 
No mkuu,kwa kuangalia life expectancy si kipimo sahihi mkuu
 

Mkuu MN,

Nakubaliana na wewe kwa asilimia 100, tumezidi blah blah!!! kibao. Tukizidiwa na Kenya tunaanza kuongelea Kibera wakati hata Tanzania tuna maeneo ambayo ni balaa kuliko hiyo Kibera. Kuna maeneo huko vijiji ni balaa tupu.

Njia pekee ya maana ya kuinua maisha ya watu wetu TZ ni through jobs creation. Ni lazima tuvute vitega uchumi mbalimbali kwa faida ya wananchi wetu. Lazima pia tuwasaidie wananchi wetu ili washiriki kwenye uchumi wa nchi yao. Bahati mbaya Watanzania wengi tuko zero kwenye hilo, wakati wenzetu Wakenya walichangamka mapema. Kinachotakiwa ni kujifunza na kuacha blah blah na badala yake tubadili maneno matupu ya hapa JF na kuyaweka kwenye vitendo. Serikali pia ihakikishe vitega uchumi toka nje vinanufaisha wote na sio kugeuka mrija wa kuibia Watanzania.

Kuhusu USA, unaweza kutafuta sababu zozote zile lakini mimi nitasema kinachotokea sasa ni rebalancing of free market.Kama unaamini kwenye free market huwezi ukaona kama regulations ndio jibu. Uchumi ni kama binadamu tu anayekula, ukila sana unavimbiwa, unapata machungu ya kuvimbiwa, baada ya hapo huna hamu tena ya kula mpaka baada ya muda unarudia hali ya kawaida (rebalancing).

Tatizo la sasa ni kwasababu limeikumba sector ya bank ambayo kwa watu wa West ni kama shamba la bibi. Kila wakisikia njaa ni kwenda kukopa tu. Mwaka 2001 mpaka 2003 ilikuwa kwenye telecom na watu wengi walipata madhara lakini sasa tumesau na watu kwenye hiyo sector wanapeta tu.

Njia ya maana kabisa kiuchumi ilikuwa kuziachia hizo bank zipate madhara ya kuvimbiwa. Kuna watu wengi wangeumia lakini baada ya muda tungerudi kwenye equilibrium. Lakini kwa mfumo wa siasa wa siku hizi sio rahisi kuruhusu hilo maana watapoteza kura. Tunachofanya ni sawa na kumpa dawa aliyevimbiwa, baada ya muda atavimbiwa tena maana anajua kuna dawa.

Bahati mbaya mimi ni mjamaa na siamini katika free market, hivyo bora kuokoa banks kama njia ya kuwasaidia wananchi walio wengi wasipate madhara.
 
ben,standard yako ya living,ni the basket of goods and services unazopata,this includes chakula,matibabu,shelter etc,etc the more you get of these services and goods,its quite obvious,life expectancy yako itapanda.kufa mapema means somehow,somewhere things are not fine
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…