Tony254,
UKUTA WA MERERANI UNAVYOMKERA JIRANI
Na Thadei Ole Mushi.
Leo Saniniu Laizer anauza Tena Jiwe la Mabilioni ya shilingi, wakati haya yakiendelea hapa Simanjiro Kuna nchi nyingine zinanuna. Jiwe la leo lina uzito wa kilo 6.63
Twende sawa!!!
Mwaka 2014 Nchi za Kenya na India ziliipita kwa mbali Tanzania kwa kusafirisha na kuuza katika soko la dunia, madini ya tanzanite ambayo yanapatikana hapa nchini pekee.
Kamishna wa Madini katika Wizara ya Nishati na Madini kwa wakati huo , Mhandisi Paul Masanja aliwaambia waandishi wa habari kwamba kwa mwaka 2013, Tanzania haikufikia hata nusu ya Kenya kwa mauzo ya madini hayo ya vito.
Kamishna Masanja alisema mwaka 2013 pekee, Kenya ilisafirisha na kuuza nje ya nchi tanzanite yenye thamani ya zaidi ya Dola 100 milioni za Marekani (Sh173 bilioni) dhidi ya Dola 38 milioni (Sh45.5 bilioni) zilizouzwa na Tanzania.
"Katika kipindi hicho cha mwaka Cha mwaka 2013, India iliuza tanzanite zenye thamani ya zaidi ya Dola za Marekani 300 milioni (Sh509 bilioni) kiasi cha baadhi ya wanunuzi wakubwa, hasa kutoka Marekani kujiuliza iwapo madini hayo yanachimbwa India," alisema Masanja.
Bila kumtaja jina, Kamishna huyo alisema mmoja wa wanunuzi wakubwa wa madini ya vito kutoka nchini Marekani aliwahi kumuuliza iwapo kuna migodi ya tanzanite India kwa sababu akifika huko hupata tanzanite bora na zenye ukubwa kuliko anayopata Tanzania.
Mwaka 2016 Marc Nkwame, Mwandishi Tanzania Daily News aliripoti kuwa Kenya iliuza tena madini ya Tanzanite njee ya mipaka yake yenye Thamani ya Dola milioni Mia Moja huku India ikifikia dola milioni 300 na Tanzania ambaye ndiye mwenye machimbo akiuza madini ya Dola million thelathini na nane tu.
Ujenzi wa ukuta wa MERERANI umekuwa shubiri kwa Kenya na India Kwani sasa wamebaki wakitizama show ya uuzaji wa madini moja kwa moja pale Merereni na Tanzania Sasa ndio inayoongoza kwa uuazaji wa madini haya ndani na nje ya nchi fuatilia link ifuatayo kuona yaliyokuwa yakiendelee kwenye sector ya madini.
Efforts to curb tanzanite smuggling make Tanzania shine - ENACT Africa
Huenda yaliwahi kupatikana mawe Mengine Makubwa zaidi ya haya lakini yalikuwa hayaonekani na Wala yalikuwa hayaliingizii Taifa kipato. Mtaelewa tu kwa nini Kuna vuguvugu Kati yetu na Jirani.
Tanzania haiwezi kufanywa Kama Congo kamwe.