Ghazwat
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 23,718
- 66,267
Familia moja katika eneo la Takaungu, Kaunti ya Kilifi inaomboleza kifo cha dereva wa Matatu kufariki nyumbani kwa mpenzi wake (mchepuko).
Kupitia mzee Shali Gona, familia hiyo inasema kifo cha Michael Kazungu, 57 nje ya nyumba ya mpenzi huyo Jumatatu kinaibua maswali mengi.
Kwenye mkasa huo Kijijini Kiwandani, mwanamke aliyekuwa na marehemu alitoweka, na kufikia jana hakuwa akipatikana kwenye simu.
Kulingana na majirani, marehemu alikuwa akiendesha matatu za kati ya Kilifi-Mombasa, alikuwa amemtembelea mwanamke huyo. Baada ya kukaa muda mchache ndani ya nyumba ghafla! akatoka mbio huku akitokwa na jasho kabla ya kuanguka na kufariki nje ya nyumba hiyo.
Msemaji wa familia Bw Brown Kahindi alisema marehemu alitoka nyumbani kwake Tezo muda wa saa tatu usiku na kumuaga mkewe kuwa anakwenda kulala mjini Kilifi ili awahi kuamka asubuhi kuanza kazi.
Aidha familia inadai kuwa kuna njama, kwa vile polisi walirekodi taarifa za mwili huo katika Mochari ya Hospitali kuu ya Kaunti kama usiokuwa na jina licha ya kuwa alikuwa na kitambulisho chake
Sasa familia hiyo inataka polisi waharakishe uchunguzi na kumsaka mwanamke huyo.
OCPD wa Kilifi Bw Alexander Makau aliwaambia wanahabari ofisini kwake kuwa hakuwa amepata taarifa hiyo. Aliahidi kuwasiliana na wanahabari pindi tu akipata habari kutoka kwa msimamizi wa kituo cha polisi Kilifi.