Ghazwat
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 23,718
- 66,267
Kiongozi wa upinzani Raila Odinga ambaye alirejea nchini Ijumaa kutoka ziara ya siku kumi Amerika, amesema atatangazia wafuasi wake hatua atakazochukua Juma hili.
Japo Bw Odinga alikataa kutaja mwelekeo atauchukua hadi majaji wa Mahakama ya Juu watoe uamuzi wao Jumatatu, aliashiria kwamba upinzani utaendelea kukabiliana na serikali.
"Safari ya ukombozi wa tatu imeanza rasmi leo", Bw Odinga aliwaambia wafuasi wake Ijumaa ambapo watu zaidi ya watano waliuawa na mali kuharibiwa wakati Polisi walipokabiliana na wafuasi waliofurika katika barabara za Nairobi kumkaribisha Odinga.
Ikiwa mahakama itatupilia mbali kesi zilizowasilishwa na aliyekuwa mbunge wa Kikome John Harun Mwau na Wanaharakati Njonjo Mue na Khelef Khalifa, Rais Mteule Uhuru Kenyatta na Naibu wake William Ruto wataapishwa kwa kipindi cha pili baadaye mwezi huu.
Updates;
Mahakama ya Juu ya Kenya yatupilia mbali kesi zilizowasilishwa kupinga uchaguzi wa marudio, imeidhinishwa ushindi wa Rais Uhuru Kenyatta
Jaji Mkuu David Maraga amesema majaji kwa kauli moja wameamua kwamba kesi zote mbili hazina msingi.