Kenya.kuna njaa sana, ila kuna kundi liko mitandaoni wakijifariji kuwa Kenya njaa hakuna

aise

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2018
Posts
5,175
Reaction score
16,488
Zaidi ya watu 800,000 wanaendelea kuumia kwa makali ya njaa na kiu kwa mujibu wa wizara ya kudhibiti majanga na utumishi wa umma ya kaunti ya Turkana.
Huyu ni mama Audan Loteng' Takwa aliye na umri wa miaka 63. Anaelezea masaibu anayopitia yeye na wanakijiji wenzake ambao wanahofia huenda wakaangamia kwa njaa iki serikali ya Kenya haitaingilia kati hali yao.
Anna Emaret anasema amekuwa akigawana chakula na mifugo wake, lakini chakula kilipoisha, wakafa.
Mama huyu ana ujauzito wa miezi sita na hajakula chochoto kwa siku tatu zilizopita.
Mariam Loolio ni ajuza mwenye umri was miaka 85. Kwa siku tano anasema hajala chochote.
Kwa mujibu wa mtazamo kuhusu uwepo wa chakula cha kutosha kwa Kenya 2019 , baadhi ya maeneo ya mashariki, kaskazini na kaskazini magharibi mwa Kenya ambapo kuna jamii za wafugaji, huenda zikakabiliwa na mzozo wa uhaba wa chakula.
Kila mara ukame unapobisha hodi, maisha ya wakaazi na mifugo wao huwa hatarini.
Mama Lakunyiko Emankor mwenye umri wa miaka 60 ni mkaazi wa kijiji cha Lotukumo katika eneo la Turkana ambalo linakabiliwa na njaa.
Wakaazi wengi katika kijiji hiki hawajatia chakula chochote mdomoni kwa muda wa karibu siku 5 zilizopita.
Serikali ya kaunti hiyo wiki iliyopita ilitoa hakikisho kwamba imeidhinisha mpango wa usaidizi kuwakinga wakaazi kutokana na madhara ya ukame uliopo.
Kwa sasa wakaazi hawa wanalazimika kutuliza makali ya njaa kwa kula matunda ya mwituni yajulikanayo kama Mkoma.
"Kuuza mifugo wakati wa mvua na kuwekeza fedha ili kujinusuru wakati wa kiangazi itasaidia pakubwa katika kuhakikisha kwamba ukame unasalia kuwa historia".
Watoto pia hawajasazwa na baa hili la njaa.
Huyu ni Mama Lakunyiko Emankor mwenye umri wa miaka 60 ni mkaazi wa kijiji cha Lotukumo.
Huyu Mzee anapumua. Tumbo halina kitu kabisa. Alipopewa maziwa kwake ilikuwa kama muujiza.
 
Wakenya achana nao katika Elimu juu ya Maslahi ya Taifa lao, ulidhani wao pia ni mburula kama sisi tusioelewa madhara ya Kutia Chumvi matukio. Umeona wapi Wakenya wakilayuka Ovyo kuhusu Shambulizi la Kigaidi la Dusit, Umeona wapi Wakenya wakitukana Serikali yao kuhusu Mgomo wa Wafanyakazi wa Viwanja vya Ndege, Umeona wapi Wakenya wakirusha Picha za Ndege zao za Kenya Airways zilizogongana Kwenye Yard ya Matengenezo, Vilevile sio Wapumbavu wa Kulalamika juu ya Baa la Njaaa linalowakumba sasa hivi.
Mweeee Mweeeeee njooo Tanzania sasa, unajua Wakenya wanatuitaje kule kwao??? Sie wanatuita MAKASUKU ayseeeee tunajua kupepeta midomo! Si wanaume si Wanawake sie Wambeaaaaaaa asikwambie mtu.
Vipi kuhusu Ndege ya ATCL kusukumwa kwa mikono pale JNIA? Vip yale mambo yetu ya Kibiti??? Vip ishu ya Watu kutekwa ilivyokuzwa mpaka Wataliii wamepungu. Inshort sisi ni Vilaza to some Extent.
 
Sijakuelewa kabisa. Au uko kwa Praise team?
 
Nimeangalia taarifa muda si mrefu Citizen Tv hali inatisha njaa kali kaskazini mwa nchi

Sent using Jamii Forums mobile app
 

na kila kizuri kilichopo tanzania mnataka kujisifia chenu kama malaya
 

Serikali ya Tanzania ni wakati wa kuzitumia mbaazi zilizokosa soko kuwasaidia wenzetu


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Weka picha ya Huyu mama Lakunyikor Emenkor
 
Weka picha ya Huyu mama Lakunyikor Emenkor
 
usituunganishe na sisi,kilaza ni wewe peke yako
bila media za kenya sisi tungejuaje kama kenya kuna njaa
 
Wewe ndiye kasuku ninani asiyejua Kenya hakuna freedom of speech ila wanapambana na hali yao.
Walio rusha zile clip za airport wakipibwa na police ni wabongo?.Walioanzisha hash tag za kuwaondoa wasomali kenya ni wabongo?.
Kimsingi ni kwamba Kenya kuna njaa muda huu jirani zetu wanateseka ukizingatia hawajapata mvua karibuni na sehemu walizopata mvua masetler wanafanya kilimo cha mirungi na mau.Pesa iliyo tolewa na serikali yao ni kidogo mno kukabiliana na janga la njaa.
 
AFADHALI NJAA YA CHAKULA KULIKO NJAA YA ALBINO
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…