Kenya kuondoa Visa kwa wageni inaweza kuwa na athari gani kwa usalama wa majirani zake?

Kenya kuondoa Visa kwa wageni inaweza kuwa na athari gani kwa usalama wa majirani zake?

LAZIMA NISEME

JF-Expert Member
Joined
Apr 5, 2015
Posts
240
Reaction score
267
Je, Kenya imeweza kutambua kwamba suala hili linaweza kuwa na matokeo tofauti kulingana na walafi wa rasilimali za Afrika na jinsi sera hiyo inavyotekelezwa na serikali inavyoshughulikia masuala ya usalama wa mipaka?

Je, Kenya imejiridhisha juu ya
  1. Kuingia kwa watu wanaotaka kufanya uhalifu?
  2. Ugaidi na Usalama wa Kitaifa?
  3. Wahamiaji haramu?
  4. Biashara haramu?
  5. Ukosefu wa Udhibiti wa Vitambulisho
Jumuiya ya Afrika Mashariki ifanye nini juu ya hatua hii ya Kenya?

Kenya wana advance sana kiuchumi kupita Tanzania. Inabidi uende Kenya kujua hii, I was dumb.
 
Tuache uoga maendeleo Ni watu tizama USA Kuna kila aina ya mtu. Ni kurekebisha tu Sheria zetu za kulinda rasilimali basi tena Bora wageni maana wazawa wanatupiga kweli rasilimali
 
Tuache uoga maendeleo Ni watu tizama USA Kuna kila aina ya mtu. Ni kurekebisha tu Sheria zetu za kulinda rasilimali basi tena Bora wageni maana wazawa wanatupiga kweli rasilimali
Kwanini USA unaingia na VIZA? na hauingii kiholela?
 
Duu, wameichoka nchi yao sasa wanataka kuifanya kama nchi za Sahelna Libya ambalo limekuwa pango la wanyang'anyi na ushaloba kwa wazamiaji wa kwenda ulaya.
Ruto aangalia uamuzi wake upya.
 
Duu, wameichoka nchi yao sasa wanataka kuifanya kama nchi za Sahelna Libya ambalo limekuwa pango la wanyang'anyi na ushaloba kwa wazamiaji wa kwenda ulaya.
Ruto aangalia uamuzi wake upya.
Ukiwa una rasilimali nyingii halafu watu wako sio competitive and unproductive lazma uhofie watu wa nje, Ila kwa wenzetu tukubali human capital yao ipo vizuri na wao hawana rasilimali nyingi sana zaidi ya kutegemea service based industries tofauti na sisi huku kwetu, rasilimali nyingi Ila SISI wananchi sio productive ndio maana tunahofia wengine wakiingia tutashindwa kupambana nao
 
Nataka nitoe maoni yangu kuhusu hili.
1. Kenya hawana cha kupoteza maana tayari nchi yao ipo mikononi mwa wakoloni so sisi majirani tunatakiwa tujiangalie sana na hawa wenzetu.

2. Mpango wa kuruhusu watu kuingia bila visa lengo lao ni kuleta watu wengi kwenye nchi yao. Lakini mtu ambaye anashindwa kuingia kwenye nchi fulani bila visa ujue uwezo wake kifedha ni mdogo. Maana yake utakaribisha watu ambao hawanafedha kuja kujaa kwenye nchi yako. Matokeo yake unaweza ukapata mtaji wa kisiasa kama utawaruhusu hao watu waweze kupiga kura. Lakini vilevile unaweza kusababisha ugomvi ndani ya nchi, kati ya wenyeji na wageni. Maana wageni nao watataka kufanya kazi zile ndogo ndogo za wenyeji.

Asante
 
  1. Usalama wa Taifa: Kuruhusu wageni kuingia bila visa kunaweza kusababisha changamoto katika kudhibiti usalama wa taifa. Kupitia mianya isiyo rasmi, watu wenye nia mbaya wanaweza kuingia na kufanya shughuli za uhalifu au kigaidi, kuathiri usalama wa ndani ya nchi.
  2. Uhamiaji Haramu: Sera ya kuruhusu wageni kuingia bila visa inaweza kuchochea uhamiaji haramu na kuongeza idadi ya watu wasio rasmi. Hii inaweza kusababisha mzigo wa kiuchumi na kijamii, pamoja na upungufu wa rasilimali za serikali.
  3. Usalama wa Afya: Bila udhibiti wa kutosha, kuruhusu wageni kuingia bila visa kunaweza kuongeza hatari ya magonjwa kusambaa. Kwa mfano, mlipuko wa magonjwa kama vile magonjwa ya kuambukiza yanaweza kuingizwa kwa urahisi na wageni wasio na uchunguzi wa kutosha.
  4. Uchumi: Kuingia kwa wageni bila visa kunaweza kusababisha hasara ya kiuchumi kwa nchi. Wageni hawa wanaweza kufanya kazi au kufanya biashara bila kutoa michango inayostahili kwa uchumi wa nchi.
  5. Mazingira: Idadi kubwa ya wageni inaweza kuwa na athari kubwa kwa mazingira, kama vile matumizi makubwa ya rasilimali za asili, uchafuzi wa mazingira, na msongamano wa miundombinu.
  6. Uzalishaji na Ajira: Kuruhusu wageni kuingia bila visa kunaweza kusababisha ushindani mkubwa katika soko la ajira. Wageni wanaweza kuchukua fursa za ajira ambazo zingeweza kuwa za wenyeji, hivyo kupunguza fursa za ajira kwa wananchi wa ndani.
  7. Mgawanyiko wa Jamii: Ongezeko la idadi ya wageni bila visa kunaweza kusababisha migongano ya kitamaduni, kijamii, na kiuchumi kati ya wageni na wenyeji. Hii inaweza kusababisha mgawanyiko wa kijamii na kutokuwepo kwa amani.
  8. Uchumi wa Chini: Kuruhusu wageni kuingia bila visa kunaweza kusababisha kupungua kwa mapato ya serikali kutokana na kukosa ada za visa na kodi nyingine za uhamiaji.
  9. Udhibiti wa Rasilimali: Kuruhusu idadi kubwa ya wageni bila visa kunaweza kuwa na athari kwa upatikanaji wa rasilimali muhimu kama maji, nishati, na chakula.
 
Ukiwa una rasilimali nyingii halafu watu wako sio competitive and unproductive lazma uhofie watu wa nje, Ila kwa wenzetu tukubali human capital yao ipo vizuri na wao hawana rasilimali nyingi sana zaidi ya kutegemea service based industries tofauti na sisi huku kwetu, rasilimali nyingi Ila SISI wananchi sio productive ndio maana tunahofia wengine wakiingia tutashindwa kupambana nao
Africa tumeimbishwa huu wimbo sana na ukichunguza kidogo tu unakuta hatuna raslimali kihivyo ukilinganisha na maeneo mengine duniani.
 
Attachments

  • 20230815_184614.jpg
    20230815_184614.jpg
    15.8 KB · Views: 4
Africa tumeimbishwa huu wimbo sana na ukichunguza kidogo tu unakuta hatuna raslimali kihivyo ukilinganisha na maeneo mengine duniani.
Vipi kuhusu utilization na kiasi kilichobaki mkuu
 
Labda wana mpango mwingine wa watu kuingia holela
Siwezi kujua ana maana gani kwa hilo
Ina maana waingie bila Visa kama watalii ama
Kwanza kuwakaribisha wageni ni jambo jema sana ila ni kudhibiti anakuja kufanya nini?
 
Ila wabongo tuna mawazo ya hovyo hovyo sana, tumekataa Dual citizenship kwa sababu za kijinga jinga hivi hivi, wakati huo wenzetu wanatupiga gapes kirahisi rahisi kama ivi sisi tunaendelea na wasiwasi wetu so called usalama. 🚮🚮
 
Vipi kuhusu utilization na kiasi kilichobaki mkuu
Hio hapo ni "total available". Natural mineral resources ni finite, tunavyozitumia zinazidi kupungua. Raslimali zilizo na thamani kubwa zaidi ni raslimali watu na 'produced capital' (majengo, mashine n.k). Tuwekeze kwenye elimu bora na afya kwa watoto wetu tupae. Hizi stori za tuna raslimali nyingi ni blabla tu. Wenzetu wana raslimali sawa na sisi ila za kwetu ni rahisi kuchuma zitakuja isha tutabaki maskini tusipo-focus kwenye raslimali watu.
 
Resources zote ni muhimu, na hakuna ubaya wa kuwa nazo in abudance, kinachojalisha ni tunazitumiaje kutoka tulipo. Hivyo tu mkuu
 
Ukiwa una rasilimali nyingii halafu watu wako sio competitive and unproductive lazma uhofie watu wa nje, Ila kwa wenzetu tukubali human capital yao ipo vizuri na wao hawana rasilimali nyingi sana zaidi ya kutegemea service based industries tofauti na sisi huku kwetu, rasilimali nyingi Ila SISI wananchi sio productive ndio maana tunahofia wengine wakiingia tutashindwa kupambana nao

Kwa kiasi fulani inaoneka ni sahihi. Lakini ukweli ni kwamba nchi ya Kenya bado ina changamoto nyingi sana, na kwa maoni yangu sidhani kufungulia mipaka na kuruhusu kila aina ya watu kuingia ndiyo itakuwa suluhu ya matatizo. Rafiki yangu Ruto inabidi apitie upya uamuzi huo.
Duniani kote, hakuna nchi inayoruhusu kila mtu wa taifa lolote aingie nchini kwao. Nimeona wanaruhusu nchi marafiki na pia zenye watu walio na tija kwa nchi inayowapokea. Kuruhusu kwa kila mtu kutoka kila nchi kuna madhara kwa Kenya yenyewe na pia majirani.
 
Back
Top Bottom