Kenya kutangaza mpango wa kuondoka Somalia katika kipindi ambacho mashambulizi ya Ashabaab yameongezeka, ina maanisha nini?

Kenya kutangaza mpango wa kuondoka Somalia katika kipindi ambacho mashambulizi ya Ashabaab yameongezeka, ina maanisha nini?

joto la jiwe

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2017
Posts
26,117
Reaction score
46,617
Al-Shabaab launches record 16 raids in Kenya within two months
Kenya iliingia Somalia mwaka 2011 baada ya Alshabaab kuanza tabia ya kuvuka mpaka na kuingia Kenya na kuwateka watalii mara kwa mara jambo lililotishia sekta ya utalii wa Kenya. Alshabaab walijibu kitendo hicho kwa kuanzisha mashambulizi dhidi ya Wakenya ndani ya ardhi ya Kenya kitendo kilichogharimu maisha ya maelfu ya wakenya na usalama wa nchi kuzorota sana.

Katika kipindi cha miezi miwili iliyopita, yaani kuanzia January, 2020, idadi ya mashambulizi yaliyofanywa na Alshabaab katika ardhi ya Kenya ni zaidi ya 16, kiwango ambacho ni kikubwa kuliko wakati wowote ule. Jambo la kushangaza ni kwamba, serikali ya Kenya imetangaza mpango wa kuondoka Somalia ktk kipindi ambacho mashambulizi yameongezeka, kinyume kabisa na malengo yaliyowapeleka Somalia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom