Kenya kutoa ruzuku ya $24 kwa raia maskini wa nchi hiyo. Tz matibabu bure ya wazee vp?

Kenya kutoa ruzuku ya $24 kwa raia maskini wa nchi hiyo. Tz matibabu bure ya wazee vp?

dosama

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2010
Posts
912
Reaction score
957
Source BBC SWAHILI

Nchi jirani ya Kenya itagharahia mpango wa kutoa dola 24 kila mwezi kwa raia wake kwa watu maskini kukaribiana na umaskini. watu ambao watafaidika ni watu wa Nairobi na Mombasa ambazo zitawasaidia katika ununuzi wa chakula na kuinua biashara zao.

My take
Hivi hapa kwetu kwanza ule mpango wa matibabu bure kwa wazee wetu yapo? vp pension za waastafuu zimeongezwa?
Na maskini wetu wanasaidiwaje na kodi zetu? mfumuko wa bei vp? au mpaka mbunge afe ndo tuone misaada
 
Source BBC SWAHILI

Nchi jirani ya Kenya itagharahia mpango wa kutoa dola 24 kwa raia wake kwa watu maskini kukaribiana na umaskini. watu ambao watafaidika ni watu wa Nairobi na Mombasa ambazo zitawasaidia katika ununuzi wa chakula na kuinua biashara zao.

My take
Hivi hapa kwetu kwanza ule mpango wa matibabu ya wazee wetu yapo? vp pension za waastafuu zimeongezwa?
Na maskini wetu wanasaidiwaje na kodi zetu? mfumuko wa bei vp
Siasa za Kenya ni ngumu.Huo ni mpango wa kuingia Ikulu ya Nairobi.
 
Siasa za Kenya ni ngumu.Huo ni mpango wa kuingia Ikulu ya Nairobi.

Angalau wao wanaonywsha njia kuliko kwetu ahadi hewa mwisho wa muhula kumbe walikuwa wanatania
 
Hongera wakenya kwa kupiga hatua hii. Labda itasaidia kuwaamsha jirani zenu wa Tanzania. Yaan pamoja na rasilimali nyingi walizo nazo bado hata hili limewashinda

Kuna chama kimoja kiliwahi kusema (kwenye kampeni za urais 2010), kitapunguza kodi kwenye zana za ujenzi na kutoa ruzuku ili watanzania waachane na nyumba za tembe watu wakadhani haiwezekan! Kumbe ilikuwa ni upofu tu wa kujitakia, kwan kuna mambo mengi zaidi ya hayo yanawezekana kwa rasilimali tulizonazo.

Nimewahi kusikia na mtoto wa shule ya msingi hapa Tanzania ana budget ya kama dola ... kwa siku. Swali ni kwamba, mbona hatuzioni? Mbona bado wanakaa chini? Mbona hawapewi chakula shuleni? Mbona wazazi wanachangia madawati, vitabu, ...? The same apply kwa matibabu ya wazee!

Hii inaonyesha kushindwa kwa sera za CCM
 
Wazee wapi wapewe matibabu bure? Kama ni hawa wanaopigwa mabomu wakiwa katika harakati za kudai haki zao stahik halafu kesho yake wanaitwa kwenda kusikiliza hotuba diamond wanaacha hata kula lunch ili wawahifoleni wasijechelewa kusikiliza na wakifika huko wanashangilia hata kabla kisemwacho hakijasemwa hawatakaa watibiwe bure hata kama bajeti yao inatengwa maana hawa walilelewa na kukuzwa enzi za chama kimeshika hatam hivyo hawawezi kudai haki zao bali wanasubiria kufikiriwa na watawala juu ya haki zao!
 
Leo asubuhi BBC katika dira ya dunia imetangaza kuwa serikali ya Kenya itaanza kutoa KSh. 2,000/= sawa na USD 25 kwa raia wake wote maskini wanaoishi chini ya KSH. 50/= kwa siku. Zoezi hili lilikwisha fanyiwa majaribio katika miji mikuu ya Nairobi na Kisumu. Sasa zoezi hili litaendelezwa katika miji mingine kama Mombasa. Fedha zitatumwa kwa kila mkenya aliyeorodheshwa kama maskini kwa kutumia M- Pesa.

Hivi karibuni Pro. Lipumba aliporejea kutoka Marekani alisema ni vema serikali ikamfungulia kila mwananchi akaunti benki ili iweze kumgawia kila mmoja wetu sehemu ya pato la Taifa inayotokana na mali asili zetu. Na akasema hii itawapa watu motisha ya kulinda mali asili na kuhakikisha hakuna hujuma yo yote.

Je kama serikali ya Kenya imeanza na kuonyesha mfano Tanzania ni nini kutakachotuzuia kufanya kama Kenya? Tafakari!
 
hiyo nyekundu nimeipenda. nzuri!
 
Mkuu umepatia. Sarakasi za siasa huko Kenya zina vituko! Chochote kinaweza semwa

quote_icon.png
By tatanyengo
Siasa za Kenya ni ngumu.Huo ni mpango wa kuingia Ikulu ya Nairobi.

Kweli Wakuu,
Wale wahanga wa kutimuliwa toka ktk mashamba/makaazi/miji/vijiji vyao baada ya uchaguzi wa 2007 Kenya bado mpaka leo March 2012 ni wakimbizi ndani ya nchi yao (IDP)na wanaishi ktk mahema, sasa hii sarakasi ya kuwapatia dolari watu masikini hii ni 'vituko vya wanasiasa wa-Kenya' kuwahadaa masikini waliojaa ktk nchi ya Kenya.
 
Hiyo itachangia kuboost ufukara¡ Kwa wak' naamini machief wengi watapiga bingo kuweka fake names..kuna uwezekano mkubwa wa pesa nyingi kupotea njiani¡kwanza why Mpesa?
 
Kweli Wakuu,
Wale wahanga wa kutimuliwa toka ktk mashamba/makaazi/miji/vijiji vyao baada ya uchaguzi wa 2007 Kenya bado mpaka leo March 2012 ni wakimbizi ndani ya nchi yao (IDP)na wanaishi ktk mahema, sasa hii sarakasi ya kuwapatia dolari watu masikini hii ni 'vituko vya wanasiasa wa-Kenya' kuwahadaa masikini waliojaa ktk nchi ya Kenya.

Sasa hutaki nao maskini wapate njia za kujikimu, ama huna imani na huamini kuwa kenya inaweza kushughulikia maskini wake. kumbe ndio ninyi mwataka waafrika tubaki daima tu misukule. kawaida kenya ina fulusi kiasi kingi cha kulisha hata maskini wa kanda ya Afrika mashariki kenya mojawepo mpaka fukara wote
 
Great job kenya!

Haiwezekani kutoa 'ruzuku' kwa kila raia masikini wa Kenya ila ni vizuri 'kuota ndoto nzuri' ukiamka unajikuta upo palepale katika lindi la umasikini.

Si tunaona Waziri Watengula amesha wapora masikini wa huku Turkana ardhi baada ya kufahamu 'kuna dalili za mafuta'.
 
As I said you will continue playing second fiddle as you as stunted by lack of vision! :biggrin:
 
Kwa haraka haraka ni idea nzuri, lakini maswali ni mengi. Serikali ina-define vipi umaskini? Ili mtu awe maskini anatakiwa atimize mambo gani? Kama ni kumsaidia mtu utaanza na yule mwenye shida zaidi au yule mwenye nafuu? Nairobi na Mombasa zina watu maskini kuliko Turkana? Kwa nini serikali isianze kutoa ruzuku kwa wazee wale wale waliokuwa wanachangiwa mahindi miezi michache iliyopita? Au tayari wameshatajirika?!!!

Wanasiasa ni watu wa kufuatilia kwa karibu, timing ya hii announcement ina uhusiano wowote na 2013 elections?
 
Tunakaribia uchaguzi mkuu............walipe kwanza hao wazee sio uchaguzi unakaribia nawe unaleta pumba tu...
 
Back
Top Bottom