Siasa za Kenya ni ngumu.Huo ni mpango wa kuingia Ikulu ya Nairobi.Source BBC SWAHILI
Nchi jirani ya Kenya itagharahia mpango wa kutoa dola 24 kwa raia wake kwa watu maskini kukaribiana na umaskini. watu ambao watafaidika ni watu wa Nairobi na Mombasa ambazo zitawasaidia katika ununuzi wa chakula na kuinua biashara zao.
My take
Hivi hapa kwetu kwanza ule mpango wa matibabu ya wazee wetu yapo? vp pension za waastafuu zimeongezwa?
Na maskini wetu wanasaidiwaje na kodi zetu? mfumuko wa bei vp
Siasa za Kenya ni ngumu.Huo ni mpango wa kuingia Ikulu ya Nairobi.
Leo asubuhi BBC katika dira ya dunia imetangaza kuwa serikali ya Kenya itaanza kutoa KSh. 2,000/= sawa na USD 25 kwa raia wake wote maskini wanaoishi chini ya KSH. 50/= kwa siku. Zoezi hili lilikwisha fanyiwa majaribio katika miji mikuu ya Nairobi na Kisumu. Sasa zoezi hili litaendelezwa katika miji mingine kama Mombasa. Fedha zitatumwa kwa kila mkenya aliyeorodheshwa kama maskini kwa kutumia M- Pesa.
Hivi karibuni Pro. Lipumba aliporejea kutoka Marekani alisema ni vema serikali ikamfungulia kila mwananchi akaunti benki ili iweze kumgawia kila mmoja wetu sehemu ya pato la Taifa inayotokana na mali asili zetu. Na akasema hii itawapa watu motisha ya kulinda mali asili na kuhakikisha hakuna hujuma yo yote.
Je kama serikali ya Kenya imeanza na kuonyesha mfano Tanzania ni nini kutakachotuzuia kufanya kama Kenya? Tafakari!
sema njia wameonyesha kwenye fryovers bwana!Angalau wao wanaonywsha njia kuliko kwetu ahadi hewa mwisho wa muhula kumbe walikuwa wanatania
Mkuu umepatia. Sarakasi za siasa huko Kenya zina vituko! Chochote kinaweza semwa
Kweli Wakuu,
Wale wahanga wa kutimuliwa toka ktk mashamba/makaazi/miji/vijiji vyao baada ya uchaguzi wa 2007 Kenya bado mpaka leo March 2012 ni wakimbizi ndani ya nchi yao (IDP)na wanaishi ktk mahema, sasa hii sarakasi ya kuwapatia dolari watu masikini hii ni 'vituko vya wanasiasa wa-Kenya' kuwahadaa masikini waliojaa ktk nchi ya Kenya.
Great job kenya!
Haiwezekani kutoa 'ruzuku' kwa kila raia masikini wa Kenya ila ni vizuri 'kuota ndoto nzuri' ukiamka unajikuta upo palepale katika lindi la umasikini.
Si tunaona Waziri Watengula amesha wapora masikini wa huku Turkana ardhi baada ya kufahamu 'kuna dalili za mafuta'.