Kenya kuwakaribisha Watu kutoka EAC mtafanikiwa kuua Mbegu ya Ukabila. Hongera sana rais Uhuru

Waterloo

JF-Expert Member
Joined
Nov 30, 2010
Posts
25,356
Reaction score
38,922
Wakenya Hamjambo?

Jana nimefuatilia katika vyombo mbali mbali vya habari Wakati Rais Uhuru alipoapishwa kuongoza tena Kenya. Nilifurahi alipotoa khotba yake na kueleza kwamba kwa sasa watu kutoka Nchi wanachama wa Jumuia yetu ya Afrika Mashariki wana Uhuru wa kuingia Kenya Kufanya kazi biashara hata kuoa au kuolewa. watahitaji tu Kitambulisho cha Utaifa.

Kwangu hii ni hatua kubwa sana katika kuimarisha siasa za Kenya ambazo kwa kiasi kikubwa zinatawaliwa na msukumo wa ukanda na ukabila.Ni matumaini yangu kwamba baada ya watu wa mataifa mengine ya jirani kuingia Kenya na kufanya shughuli zao kwa kiasi kikubwa kabisa mbegu ya ukabila inaweza kupungua au kimalizika kabisa. Heko rais Uhuru hapa umefanya Jambo la maana sana.

Hongereni sana Majirani zangu Wakenya sasa Mpige kazi Siasa wekeni Pembeni.
 
Wakenya wana msemo wao, "Mombasa si Kenya ". Sasa kama wa Mombasa tu wanawatenga wewe lete pua yako kizembe zembe uone unavyotengwa.
Utaona rangi halisi ya mkenya ikifika wakati wa kuanzisha sarafu moja ya EA. Hapo agenda ya EA integration hutasikia wakiipigia debe.
 
Hivi ukabila Tanzania haupo imetupa faida gani? Maana tunaowaita wakabila wanatuzidi maendeleo.
Hata makabila ya Tanzania yenye kujitambua ndio yenye maendeleo.
Tuliumbwa tukiwa Wachaga, Wakikuyu au wapare hii Tanzania Kenya ni mazao ya mkoloni
 
Kaka hebu tuambie maana ya maendeleo kamusi yako inasomaje?
 
Wakenya Hamjambo?

Jana nimefuatilia katika vyombo mbali mbali vya habari Wakati Rais Uhuru alipoapishwa kuongoza tena Kenya. Nilifurahi alipotoa khotba yake na kueleza kwamba kwa sasa watu kutoka Nchi wanachama wa Jumuia yetu ya Afrika Mashariki wana Uhuru wa kuingia Kenya Kufanya kazi biashara hata kuoa au kuolewa. watahitaji tu Kitambulisho cha Utaifa.

Kwangu hii ni hatua kubwa sana katika kuimarisha siasa za Kenya ambazo kwa kiasi kikubwa zinatawaliwa na msukumo wa ukanda na ukabila.Ni matumaini yangu kwamba baada ya watu wa mataifa mengine ya jirani kuingia Kenya na kufanya shughuli zao kwa kiasi kikubwa kabisa mbegu ya ukabila inaweza kupungua au kimalizika kabisa. Heko rais Uhuru hapa umefanya Jambo la maana sana.

Hongereni sana Majirani zangu Wakenya sasa Mpige kazi Siasa wekeni Pembeni.

Hauna akili kama Uhuru Kenya!
 
Back
Top Bottom