Kanungila Karim
JF-Expert Member
- Apr 29, 2016
- 20,743
- 25,564
Machakos. Kenya. Mwili wa mwanaume mmoja kutoka kijijini Ndelekeni, Masinga Kaunti ya Machakos umekwama mochari kwa miaka 15 baada ya mkewe kuukataa akidai kwamba mume wake angali hai na atarejea nyumbani siku moja.
Stephen Nthuku alifariki dunia miaka 15 iliyopita baada ya kuuawa katika hali ya kutatanisha nyumbani kwake.
Mwanaume huyo aliyekuwa akiishi jijini Mombasa ambaye alikuwa akifanya vibarua vidogovidogo kwa lengo la kujipatia kipato alifikwa na umauti miaka 15 iliyopita baada ya kuvamiwa na genge la watu na kumuua.
Inadaiwa kuwa kabla ya kifo chake Desemba mwaka 2003 siku moja mwanaume huyo alirejea nyumbani na kumkuta mkewe, Stellamaris Nthuku akiwa na mwanamume mwingine nyumbani kwake.
Hata hivyo, baada ya tukio hilo mwanaume huyo anadaiwa kuondoka nyumbani kwake na kwenda kulala kwa ndugu yake kwa kile kinachodaiwa kushindwa kupambana na mgoni wake ambaye alikuwa mtu wa miraba minne.
Kwa mujibu wa gazeti la Taifa Leo la Kenya, kesho yake mwanaume huyo aliwaeleza jamaa zake na kumshauri kwenda kuripoti katika Baraza la wazee wa ukoo wa Amutei na kutekeleza hilo.
“Wazee waliandamana hadi nyumbani kwa Nthuku kwenda kumtakasa, lakini walipofika, Stellamaris alijitetea kuwa mumewe ndiyo amesababisha hayo kwa kuwa amekuwa na tabia ya kumfanyia vioja vya kutisha.
Hata hivyo, kesi hiyo haikufikiwa muafaka kutokana na mwanamke huyo kuvua nguo za ndani na kubaki mtupu kisha kuwakimbiza wazee hao huku akiwamwagia maji.
Kufuatia tukio hilo, mwanaume huyo alifungua kesi na kutaka mahakama ivunje ndoa hiyo lakini kabla ya talaka hiyo kutolewa mwanaume huyo aliuawa.
Kwa mujibu wa gazeti hilo, baada ya mwanaume huyo kuuawa mwili wake ulihifadhiwa katika Mochari ya City jijini Nairobi na mwanamke huyo alikataa kwenda kuuchukua kwa kile alichodai kuwa mumewe bado yupo hai.
Ndugu wa marehemu huyo walifungua kesi na kudai kuwa kaka yao alipigwa na kifaa butu kichwani na mwili wake kutupwa chooni. Baadaye walikodisha mkokoteni na kutupa maiti hiyo katika msitu wa B2 Yatta.
Hata hivyo, katika ushahidi wake, Mkemia wa Serikali alishindwa kubaini ikiwa mwili huo ulikuwa kweli wa Nthuku kwani alisema kuwa mifupa ya Marehemu iliyoko katika mochari ya City haikutoa matokeo sahihi ya DNA.
Stellamaris ambaye sasa anakabiliwa na kesi ya mauaji, alisisitiza kuwa maiti hiyo si ya mumewe huku akisema kwamba ana matumaini atarejea nyumbani siku moja.
Kwa sasa mwili wa mwanaume huyo unaendelea kuhifadhiwa katika mochwari hiyo pale maiti hiyo itakapotambuliwa.
Credit : Mwananchi