Kenya: Mfanyakazi atoweka baada ya kutumia fedha za bosi wake kubet na kuliwa

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Raia wa Kenya, Robert M'munoru mwenye umri wa miaka 20 kutoka Kaunti ya Lamu ametoweka na hajulikani alipo hadi sasa baada ya kutumia pesa za Boss wake kuchezea mchezo wa bahati nasibu (bettin) na fedha zote Ksh. 190,000 ( Tsh. Mil 3.8) zikaliwa

Robert ambaye ametoweka tangu November 28,2021 ameacha ujumbe dukani kwa Boss wake ambako amechukua fedha hizo ambapo kwenye ujumbe huo amekiri kutumia fedha za dukani kuchezea bahati nasibu na kusema hiyo ndio sababu ya kukimbia.

Robert alianzia Kituo cha Polisi ambako aliandika maelezo kwa Polisi akikiri kutumia fedha za Boss wake kabla ya kutoweka ambapo aliomba Boss wake apewe shamba lake lililopo Meru kama fidia na aliacha pia simu na nguo zake dukani.

Familia ya Robert inasema kama Robert atabainika kuwa amefariki Kampuni ya betting inapaswa kushughulikia mazishi yake na wakikataa Serikali itapaswa kubeba majukumu hayo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…